Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,197
- 128,160
Comrade vaa barakoa.Haya mambo ya Maombi Rais alitakiwa yeye atao tamka kuomba watu wafanye Maombi ya Taifa badala Yake Rais anaunda Tume .
Yupo pekee yake Ikulu anavaa Barakoa,
Akiwa Na mgeni wapo 2 Ikulu kwenye mazungumzo mgeni kavaa barakoa na yeye anavaa barakoa. Akivaaa mmoja Barakoa inatosha
Sijajua wataalamu wa AFYA wanamahauri vipi
mji gani huo acha kuongopea dini bwana?Hata wewe umekosea. Sio lazima maombi yaongozwe na shehe. Kuna miji haina hata shehe mmoja lkn miskiti ipo.
Wazaramo hawaishi shambaMzaramo hata awe na PhD lazima awe na ushamba Fulani. Wangapi mnamkumbuka Malima na Msabaha?
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais muungano na mazingira, Suleiman Jaffo ameongoza maombi ya kumwombea rais Samia Suluhu pamoja na Taifa kuepuka ugonjwa hatari wa Corona na kuzitaka taasisi zingine za dini hapa nchini kusimamia amani ya nchi .
Akiongea wakati wa maombi hayo yaliyofanyika makao makuu ya taasisi ya dini ya kiislamu ya Twariqa mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro waziri Jaffo amesema ipo haja kwa taasisi zote za dini hapa nchini kuliombea taifa kuepuka mifarakano inayoweza kuhatarisha amani ya nchi.
Mzaramo hata awe na PhD lazima awe na ushamba Fulani. Wangapi mnamkumbuka Malima na Msabaha? π π€£
Mburula mwenzio huyoNyungu zimeishia wapi?
Kamanda mbwakachoka!Mburula mwenzio huyo
πππKamanda mbwakachoka!
Barakoa zinafanya kazi pale kila mtu anapovaa. Nadhani hujui barakoa zinasaidiaje kwenye kupunguza kuenea kwa corona.Haya mambo ya Maombi Rais alitakiwa yeye atao tamka kuomba watu wafanye Maombi ya Taifa badala Yake Rais anaunda Tume .
Yupo pekee yake Ikulu anavaa Barakoa
Akiwa Na mgeni wapo 2 Ikulu kwenye mazungumzo mgeni kavaa barakoa na yeye anavaa barakoa. Akivaaa mmoja Barakoa inatosha
Sijajua wataalamu wa AFYA wanamahauri vipi
Fanya utafiti wako vizuri,kuna kabila corona imeleta vifo vingi mno,ingekuwa kuwa na wake wengi ni moja ya sababu,basi wapemba wangeathirika zaidi.Huyu si ndio alianzisha NYUNGU day? Hawa wazaramo taabu sana!! Ukiwa na wake watatu chances za kuambukizwa corona ni kubwa kuliko ukiwa na mke mmoja; hasa hawa wazaramo na wakwere wanaoshinda kucheza ngoma!
Kama Maneromango Ni mjini haya.Wazaramo hawaishi shamba
Hii Nchi Mungu aliingilia kati isitumbukie Shimoni kwa Kumtwaa MwendazakeWaziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais muungano na mazingira, Suleiman Jaffo ameongoza maombi ya kumwombea rais Samia Suluhu pamoja na Taifa kuepuka ugonjwa hatari wa Corona na kuzitaka taasisi zingine za dini hapa nchini kusimamia amani ya nchi .
Akiongea wakati wa maombi hayo yaliyofanyika makao makuu ya taasisi ya dini ya kiislamu ya Twariqa mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro waziri Jaffo amesema ipo haja kwa taasisi zote za dini hapa nchini kuliombea taifa kuepuka mifarakano inayoweza kuhatarisha amani ya nchi.
Alisema uamuzi uliofanywa na taasisi ya Twariqa kuliombea taifa ni Jambo jema linalopaswa kuigw na taasisi zingine za dini chini ili kuepuka ugonjwa hatari wa Corona ambao umelikumba taifa na dunia kwa ujumla.
Akitolea mfano nguvu ya maombi ilivyokimbiza ugonjwa wa Corona hapa nchini ,pamoja na kimbunga hatari cha Jobo kilichotishia amani ya nchi ni kielelezo kwamba ipo haja kwa viongozi wa dini kuzidisha nguvu ya maombi ili taifa liendelee kubaki salama.
Awali katibu wa taasisi hiyo ya Twariqa Yahaya Mkindi alisema lengo la kuwakutanisha waislamu na waziri Jaffo katika makao makuu ya taasisi hiyo ni kuliombea Taifa kuepuka ugonjwa hatari wa korona sanjari na kumwombea rais Samia Suluhu Hasan aweze kuliongoza Taifa vema akiwa na hofu ya mungu Kama mwanamke wa kwanza Tanzania kuwa rais wa kike.
"Tumekutana hapa kwa ajili ya kuombea janga la gonjwa wa covd 19 likae mbali na Tanzania pamoja na kumwombea rais Samia Suluhu Kama mwanamke wa kwanza kuliongoza Taifa la Tanznaia"alisema
Aidha katika hatua nyingine katibu mkuu Mkindi alisema taasisi hiyo ipo katika hatua ya mchakato wa ujenzi wa kituo Cha afya Cha mama na Mtoto kitakachosaidia akina mama kujifungua na kuepusha Vifo visivyo vya lazima.
Kwa upande wake msemaji mkuu wa Twariqa sheikh Haruna Hussein aliwataka waislam kuendelea kuwa wamoja na kuepuka mifarakano isiyo na tija inayotokana na kugombea madaraka kwa waislamu wasiotaka mabadiliko kuendelea kung'ang'ania madarakani.
Alisema maombi hayo yaliyowakutanisha pia viongozi wa wakuu wilaya ya Moshi mjini na meya wa Juma Shaibu Hussein alisema Amani ni tunu ya nchi hivyo kila kiongozi anapaswa kudumisha Amani na kuielezwa Amani kwa jamii yote inayomzunguka.
Ends...