Waziri Jafo asema wananchi 595 kulipwa fidia ya Tsh. Bilioni 6.26 Engaruka, Monduli

Waziri Jafo asema wananchi 595 kulipwa fidia ya Tsh. Bilioni 6.26 Engaruka, Monduli

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) amesema kuwa wananchi 595 waliofanyiwa uhakiki wa mali katika eneo la mradi wa Engaruka (Monduli) wanalipwa jumla ya shilingi bilioni 6.26

Amebainisha hayo Januari 09, 2025 jijini Arusha akihojiwa asubuhi na Azam Tv na kusema kuwa "Agosti 24, 2024 alifika katika eneo la Engaruka na kukutana na wananchi kwa niaba ya Serikali na kuahidi kuwa Serikali ni sikivu na itawalipa fidia hivi karibuni".

Aidha, Dkt. Jafo amesema mradi wa Engaruka utakuwa na faida kubwa kwa wananchi kwa kufungua fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ajira na kukuza uchumi wa mtu mmojammoja na Serikali kwa ujumla.

Screenshot 2025-01-09 at 22-23-18 Shammah Fm (@shammahfmtz) • Instagram photos and videos.png
 
Back
Top Bottom