Waziri Jafo: Wananchi nunueni Majokofu mapya yale ya mitumba yanachafua hali ya hewa!

Na hela ya kutop up wanatuongezea kwa njia ipi mobile money au Bank?
 
Badala ya kuwaambia wananchi aongee na Taasisi husika ili kuzuia kupunguza uagizwaji wa majokofu hayo, na kupunguza kodi kwenye mapya..
 
Hajui huyo, msamehe. Gas hiyo haikai kwenye mazingira. Inapaa juu na kwenda kuitafuna ozone layer, inayokinga mionzi hatari toka kwenye jua (utraviolet rays) ambayo ikitufikia huleta hatari nyingi, ikiwemo kansa ya ngozi, kuzeeka ngozi mapema, na matatizo ya macho. R12 na 22 au Freone 12 na 22 Ulaya kwa sasa zipo ni kwenye makumbusho ya maabara. R134a ndio gas inayotumika kwa sasa.
 
Mi naomba kuuliza majokofu ndio kitu gani
Mafriji mkuu , nimenunua jipya zaidi ya 1m, haya yazamani yanamaliza sana umeme wa LUKU .
Lakini wangapi wanaweza kununua mpya.

Mwaka wa sita huu hawatoi ajira.

Mazingira hayawezi kutunzwa na yakapendeza kwenye ufukara na maisha duni kama Tanzania.

Tunaposema CCM wameshindwa wapishe hii ndio maana yake.
Huko vijijini watu wanakata tu miti hovyo kutengeza mikaa wanafukuza mvua, tafuteni mbadala wa mkaa. Hii nchi ipo kwenye hali mbaya kimazingira.
 
Ni kweli kabisa, lakini kosa si la wanunuzi kosa ni wale wanaoruhusu bidhaa zisizo na ubora kuingizwa nchini.
Hata hivyo Waziri wa Mazingira anao wajibu wa kusaidia walau kwa kupiga marufuku uingizwaji wa bidhaa zinazochafua mazingira.
 
Kulea miti halihitaji utafiti. Kupika ni lazima. Serikali inakamata wauza mkaa bila kuweka mbadala ya nishati mbadala. Serikali ikiondoa kodi kwenye gas, majiko na vifaa vyake, ikashusha bei ya umeme majumbani, hakuna atakae pikia mkaa. Miaka 10 baadae mbao zitakosa wanunuzi na tuta export na kupata hela za kigeni. Serikali kubariki kuongeza bei ya gas na umeme ni uendawazimu.
 
Ni kweli kabisa, lakini kosa si la wanunuzi kosa ni wale wanaoruhusu bidhaa zisizo na ubora kuingizwa nchini.
Hata hivyo Waziri wa Mazingira anao wajibu wa kusaidia walau kwa kupiga marufuku uingizwaji wa bidhaa zinazochafua mazingira.
Waziri anakumbuka shula majogoo.
 
Huoni kama wewe ndo kilaza aisee,au hujui CFCs toka ktk mafridge/AC ndo zinachangia KWA kiasi kikubwa kuharbu ozone?

Hebu piga shule kwanza Kisha ndo ujibu thread za kitaaluma
Kinachowafanya wasikataze hizo friji za mtumba ni nini??? Tatizo umekurupuka kunijibu, lengo langu sio kukataa uhabiribifu unaotokana na hizo friji... Kwanini wao wasichukue hatua kama mamlaka??? Kwanini wasiongeze kodi kwenye za mtumba na waounguze kwenye friji mpya ili kutimiza hiyo azma yake badala ya kupayuka tu watu wasinunue kitu ambacho ni ngumu kutekelezeka???
 
Hivi hata ukinunua jipya si baada ya muda linaitwa la zamani tuu[emoji848][emoji848]
 
R134 na yenyewe wameacha kuitumia kwenye latest fridge. Fridge latest ya mtumba inatumia R600 siku hizi

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Waambie wawaambie na wake zao wanaofanya biashara ya mitumba waache!
 
Vipi anasemaje kuhusu nguo za mitumba na magari ya mitumba kuhusu kuchafua mazingira na.hewa ya ukaa. Tuba.wanasiasa mamburulaz kweli kweli. Shibe mwanamalevya

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Asante mkuu, mi ndio Mara ya kwanza kushika neno majokofu ila leo nimejifunza,Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…