Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Jenista Mhagama akabidhi vifaa kuimarisha kitengo cha mawasiliano na elimu ya afya kwa umma
Waziri Mhagama wakati akikabidhi vifaa hivyo amewataka watumiaji wa vifaa hivyo kuvitunza na kuvitumia vizuri ili kufikia lengo lililokusudiwa la kuihabarisha jamii katika masuala ya Sekta ya Afya.
"Twendeni tukavitunze vifaa hivi, kwa kuwa huu ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ambapo wananchi wanatakiwa kufaidika kwa kupata Habari mbalimbali za Afya pamoja na Elimu ya Afya." Amesema Waziri Mhagama.
Waziri Mhagama amewataka wataalam hao kufanya kazi zenye ubunifu na viwango vya juu huku maudhui yatakayozalishwa yawe yamezingatia maadili, mila na desturi za Kitanzania.
Vifaa hivyo ni pamoja na Camera, Boom Mike, Mixer, Laptop, Macbook, Drone's, Tripod Stand pamoja na vifaa vingine vya Studio ambavyo vyote vimenunuliwa na Wizara.