Waziri Jenista Mhagama bado kuna changamoto za kiutendaji hapo makao makuu ya NHIF. Shirikiana na TIRA kuokoa jahazi

Waziri Jenista Mhagama bado kuna changamoto za kiutendaji hapo makao makuu ya NHIF. Shirikiana na TIRA kuokoa jahazi

Doctor Mama Amon

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
2,089
Reaction score
2,725
Mheshimiwa Waziri,

Napenda kukuandikia tena kuhusu changamoto za utendaji wa kazi katika Makao Makuu ya NHIF, Dodoma. Bado Ombwe la Kanuni Zinazotabirika Linasumbua Makao Makuu ya NHIF. Hivyo, nakuandikia kukuomba ushirikiane na TIRA kuokoa jahazi

Utangulizi

Tarehe 20 Oktoba 2024 niliandika makala ya kutoa Wito kwa Waziri Mhagama na Mkurugenzi wa NHIF kuhakikisha kwamba NHIF wanaacha kufanya kazi kiswahili.

Badala yake nilipendekeza kwamba NHIF wanapaswa kuandaa na kufanya kazi kwa mujibu wa Kanuni zinazozingatia “Service Delivery Cycle" inayofahamika kwa wadau wote na yenye kutabirika.

Tarehe 21 Novemba 2024 Mamlaka ya Kusimamia Mifuko ya Bima nchini, yaani Tanzania Insurance Regulatoru Authority (TIRA), ilitoa taarifa kwa umma ("Public Notice").

Tulijulishwa kuwa tayari uongozi wa NHIF umeagizwa kutekeleza majukumu yake kulingana na matakwa ya sheria, kanuni na taratibu za utoaji wa huduma za bima nchini.

Sheria zilizotajwa na tangazo la TIRA ni "Universal Health Insurance Act (2023)," "Universal Health Insurance Regulations (2024)," na "The Insurance Act (2009)."

NHIF waliagizwa kuwa wamezingatia kwa ukamilifu miongozo hii ya kisheria na kikanuni kabla ya tarehe 31 Desemba 2025.

1741543476661.png

Katika muktadha huu, tarehe 27 Desemba 2024 niliandika makala ya kumpongeza Dkt. Irene Isaka, Mkurugenzi wa NHIF, kwa kuanza mwaka 2025 kwa kishindo kutokana na Kabuni vifurushi vipya vya Serengeti, Ngorongoro, na Toto Afya Kadi.

Tatizo lililopo kwa sasa

Na sasa, leo napenda kukupa mrejesho kuhusu ninachokiona kikiendelea ndani ya Makao makuu ya NHIF kuhusiana na mantiki ya maagizo ya TIRA. Nimethibitisha yafuatayo mpaka sasa:

1. Kwamba, "Universal Health Insurance Regulations (2024)" zilizotajwa na TIRA hazijaandaliwa mpaka tarehe ya leo, na bado kuna miezi 10 mbeleni ili tujiridhishe kuhusu maandalizi yake, kama tukifuata mwongozo wa TIRA.

2. Kwamba, "NHIF regulations (2022)" zinazopaswa kutumika sasa hivi wakati wa kipindi cha mpito kuelekea ukomo wa 31 Desemba 2025 hazipo kwenye tovuti rasmi ya NHIF, na hazifuatwi na watendaji wengi wa makao makuu, na hivyo wengi wao kujikuta wanafanya kazi ya "stakeholders expectations management" kwa kubahatisha badala ya kuongozwa na kanuni hizo.

3. Kwamba, ombwe la kikanuni linalowakabili watendaji wa makao makuu ya NHIF linatoa mwanya kwa wasaidizi wa MKurugenzi Mkuu, kama vile Mkuu wa Idara ya kuchunguza udanganyifu na Idara ya Huduma za Tiba na Mafunzo (DMTS) kujipa mamlaka yakutunga kanuni holela zinazoongoza utendaji kazi wao.

Mfano, kazi ya "ukaguzi" lazima iongozwe na kanuni zinazojulikana kwa mkaguzi na mkaguliwa, maana ukaguzi wa mazingatio ya kikanuni (compliance audit) lazima uongozwe na kanuni, ili tuweze kutofautisha watiifu na wakaidi. Hili jambo halipo kwa sasa ndani ya Makao Makuu ya NHIF. Wakaguzi wanaongozwa na utaratibu wa mbele kwa mbele tu.

4. Kwamba, mkuu wa kitengo cha ukaguzi cha makao makuu amejipatia mamlaka ya kupiga veto maamuzi ya kamati ya huduma za afya wakati yeye ni mjumbe mmoja mwenye kura moja ya maamuzi katika kamati hiyo. Jambo hili linaiyumbisha ofisi ya DG kwani inakuwa na kigugumizi cha kutoa kibali (approval) kwa yale maamuzi yaliyopigwa veto na mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi hata kama hoja zake zilikataliwa ba wajumbe wa kamati.

Mfano, kuna maamuzi yalifanyika Januari 2025 kwenye kikao cha 144 cha Kamati ya Huduma ya Afya na hayakuwa yametekelezwa mpaka kilipoitishwa kikao kingine cha 145. Kikao cha 145 cha kamati ya huduma za afya kilifanyika tareh 19 Februari 2025.

Kwenye vikao hivi, maombi yote ya watoa huduma yalipitishwa. Miniti za vikao zilipelekwa kwa DG kwa wakati ili atoe vibali (approval) vya utekelezwaji wa mamuzi hayo.

Lakini, baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Fraud na watendaji katika ofisi ya DMTS waliokuwa sehemu ya Kamati ya Huduma za Afya iliyofanya maamuzi ya pamoja wakatangulia kwa DG kusema baadhi ya waombaji wasipewe kibali hata kama Kamati imeruhusu.

Mpaka leo waombaji hao wamepigwa pini bila kufuata utaratibu rasmi unaojulikana kwa wadau wote wa NHIF.

Tatizo kama hili limekuwa likijitokeza kwenye vikao vya nyuma pia. Ndilo tatizo nalirejea kama USWAHILI unaopaswa kuepukwa na NHIF.

Kwa sababu hii sasa hitimisho mwafaka ni kwamba practically speaking the real Director General wa NHIF ni DR. Rose wakati Dr. Irene Isaka ni ceremonial Director General. Lakini taasisi kubwa kama NHIF haipaswi kuendeshwa kiswahili namna hiyo.

5. Na kwa mara mbili sasa DG mpya wa NHIF, Dr. Irene Isaka, amekubaliana na uvurugaji unaofanywa na Mkuu wa kitengo cha uchunguzi, Dr. Rose.

Ni hivi: Mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi ni mjumbe wa Kamati ya Huduma za Afya. Kamati hii hukutana mara moja kila mwezi kufanyaa maamuzi kide.okrasis na kumshauri DG kuhusu vibali vya watoa huduma. Kila mjumbe wa Kamati hii akiwemo mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi anayo kura moja.

Maajabu ni kwamba mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi akijenga hoja yake ya kupinga jambo kwenye ngazi ya kamati ya huduma za afya na hoja yake ikakataliwa kwa kukosa ushahidi baada ya hapo anawahi kwa DG kuweka kauzibe.

Nina ushahidi kwamba DG mpya amekubaliana na uswahili huu mara mbili mpaka sasa badala ya kumwambia "Dr. Nanihii, hoja zako unapaswa uwe unazijenga ndani ya kamati na sio nje ya kamati."

Kwa vile DG anakaribisha majungu ofisini kwake huo ni udhaifu. Anapaswa kusimama imara kwa mujibu wa kanuni. Kama kanuni hazipo ni jukumu lake kuhakikisha kuwa zinakuwepo.

Mapendekezo ya kiutekelezaji

Mheshimiwa Waziri, kutokana na changamoto hizi, ninayo mapendekezo mahsusi kama ifuatavyo:

1. TIRA waangalie uwezekano wa kufupisha muda wa mpito walioutoa kwa NHIF kutoka tarehe 31 Desemba 2025 hadi 31 Julai 2025. Kanuni thabiti kwa ajili ya kuongoza kazi za NHIF zinahitajika haraka sana.

2. Mkurugenzi wa NHIF aagizwe kuweka wazi Kanuni za NHIF za mwaka 2022, na Kanuni zingine baki zinazotumika kwa sasa, kwa kuzipakia kwenye tovuti ya NHIF ili wadau wote wa NHIF wajue wanahudumiwa kwa mujibu wa kanuni gani. Tovuti ya sasa haina hata sheria mama za NHIF. Jambo hili sio sawa. Mfano mzuri ni Sheria na Kanuni za TMDA zinavyoonekana kwenye tovuti yake.

1741348882169.png

Dr. Rose, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi, NHIF Makao Makuu, Tanzania

3. Kitengo cha ukaguzi wa udanganyifu kiweke bayana kanuni zake kwa wadau wanaokaguliwa ili kiweze kuaminika kwamba kinatenda haki. Mfano mzuri ni Kanuni za TMDA zilizoko kwenye tovuti yake. Aidha taarifa za taasisi inayoomba kutoa huduma hazipaswi kuchukuliwa kama siri dhidi ya taasisi hiyu, kama inavyofanyika kwa sasa.

Kulingana na majukumu yake yanayohitaji usaili na mahojiano na watuhumiwa yanayofuatiwa na countersigning of final report kitengo hiki hakiwezi na hakipaswi kufanya kazi kwa mtindo wa kikachero hata kidogo.

Kanuni ya uwazi izingatiwe mara zote Katika utendaji kazi wa kitengo hiki.

Mfano: Inapokuwa inachunguzwa taasisi iambiwe tunakuchunguza katika maeneo haya na yale, ili taasisi ipate sababu nzuri ya kutoa ushirikiano stahiki kwa wakati na hivyo kuharakisha mchakato wa ukaguzi.

Kazi ya ukaguzi ni tofauti na kazi ya matambiko ya kiiukoo ambayo hufanywa siri dhidi ya watu wote baki wasio wanaukoo. Ujumbe huu umfikie Dr. Rose Mkuu wa Kitengo cha ukaguzi makao makuu.

1741348805858.png

Dkt. David Mwenesano, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Mafunzo, NHIF Makao Makuu, Tanzania

4. Kitengo cha Huduma za Tiba na Mafunzo kwa watoa huduma wanaohudumia wanachama wa NHIF kinapaswa kujihimu kwa kuhakikisha kwamba urefu wa "service delivery cycle" tangu maombi ya mtoa huduma yanapofika ofisini mpaka anapopata kibali cha kutoa huduma umetamkwa kikanuni.

Muda huu haupaswi kuwa open-ended kama ilivyo sasa, kiasi cha kuwafanya wadau kutilia mashaka weledi wa DG anayesimamia huduma zote za NHIF.

Mfano, DMTS akisha saini mkataba anapaswa kuhakikisha kwamba "wino" alioumwaga kwenye mkataba unaanza kumnufaisha mwanachma wa NHIF mara moja.

Sio sawa mkataba unasainiwa na DMTS tarehe 07 Februari 2025 na hadi tarehe 07 Machi 2025 bado mtoa huduma hajapata kibali cha kuanza kutoa huduma na bado DMTS anakaa kimya kana kwamba kila kitu kiko shwari.

Mtu anayekalia kiti cha DMTS anapaswa kufanya kazi kwa ukaribu na DG na DMTS hapaswi kukubali kitengo cha Ukaguzi kuchelewesha utekelezaji wa maamuzi yake muhimu na hivyo kumfanya yeye aonekane anamhujumu DG. Maneno haya yamfikie Dr. Mwenesano, Mkuu wa Idara hii.

1741768283725.png

Dr. Irene Isaka, DG mpya wa NHIF

5. DG wa sasa, Dkt. Irene Isaka, ambaye ni mgeni ofisini akumbushwe kwamba anao wajibu mahsusi kama ifuatavyo:

Mosi, DG anao wajibu wa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa kanuni na sio kwa kusikiliza majungu ya watu wanaojipendekeza kwake kama anavyofanya mwenyekiti wa kamati ya ukaguzu. Uswahili wa namna hii upigwe marufuku.

Na pili, DG anao wajibu wa kupanga timu yake kulingana na hati ya majukumu yake, kwa maana kwamba, wasaidizi wake wote ambao anaona wanamsaidia kwa shingo upande, na wakati mwingine kumpotosha kwa makusudi, awaweke pembeni.

Kwa sasa kasi ya utendaji wa ofisi ya DG inahitaji wasaidizi wenye mtazamo chanya kuhusu ofisi hiyo.

Napendekeza kwamba, wasaidi wote waliokuwa wanainyemelea nafasi ya DG wanajitahidi kumkwamisha DG mpya kwa makusudi.

Lakini naona kuwa yeye DG hajafahamu ukweli huu maana anapewa ushauri hatari na anaukumbatia bila kujiuliza mara mbili.

Kwa mfano najiuliza: Kanuni gani zinampa mamlaka Mkuu wa kitengo cha ukaguzi kuyapiga veto maamuzi halali ya Kamati ya Huduma za Afya wakati yeye ni mjumbe wa kamati hiyo mwenye kura moja kama walivyo wajumbe wengine na anakuwa ameshiriki kupitisha maamuzi yale anayoamua kuyapinga nje ya kikao? Haya ni maajabu!

Vurugu za aina hii zinapaswa kukomeshwa haraka Ili kulinda heshima ya taasisi inayoitwa NHIF. Dawa yake ni Kanuni, miongozo na taratibu zilizo wazi kwa wadau wote. Tabia ya kufanya kazi kwa kuviziana haifai maana inapingana na misingi ya utawala bora.

6. Na mwisho, ni kuhusu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Afya inayopitisha maombi ya watoa huduma ili kufungua mlango kwa DMTS kusaini mikataba yao.

Kwa sasa Mwenyekiti wa Kamati hii sio DMTS. Ni mtu baki. Anaitwa Mr. Maganga. Jambo hili sio sawa.

Napendekeza kwamba DMTS automatically awe Mwenyekiti wa Kamati hii kusudi aweze kufuatilia vizuri zaidi maamuzi ya Kamati ya Huduma za Afya baada ya kikao.

Ni hayo tu kwa leo.

Na baada ya kusema hayo, nakutakia ufuatiliaji na utekelezaji mwema wa majukumu yako ya kulijenga Taifa kupitia NHIF

Dr. Mama Amon,
"Sumbawanga Town"
S.L.P P/Bag
Sumbawanga.
 
Back
Top Bottom