Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
TAARIFA KWA UMMA
UZINDUZI WA MIFUMO NA KIFURUSHI CHA TOTO AFYA KADI (TAK)
Desemba 06, 2024, DodomaUZINDUZI WA MIFUMO NA KIFURUSHI CHA TOTO AFYA KADI (TAK)
1. Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama (Mb) anatarajia kuzindua Mfumo wa uandikishaji Wanachama, Mfumo wa Uchakataji Madai na Kifurushi cha Toto Afya Kadi Desemba 17, 2024. Uzinduzi wa Mifumo unafanyika baada ya Mfuko kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha Mifumo ya Serikali inasomana.
2. Aidha kwa upande wa Toto Afya Kadi, Mfuko umefanya marejeo ya kifurushi hicho kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kundi la watoto chini ya umri wa miaka 18, hali ya kipato cha wananchi pamoja na hali ya Mfuko. Kutokana na hayo, mpango huo wa Toto Afya Kadi utazinduliwa rasmi kwa tarehe tajwa hapo juu.
3. Kwa sasa Mfuko unaendelea na utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote hususan katika usajili wa wanachama kupitia makundi mbalimbali ikiwemo kundi la Wanafunzi kuanzia ngazi ya Awali hadi Chuo Kikuu kwa gharama ya shilingi 50,400/= tu.
4. Mfuko unatoa rai kwa wananchi kuendelea kujiunga ili kuwa na uhakika wa huduma za matibabu wakati wowote bila kikwazo cha fedha kupitia mtandao mpana wa vituo zaidi ya 10,000 vya kutolea huduma nchi nzima.
Imetolewa na;
Idara ya Uhusiano kwa Umma
MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)
Idara ya Uhusiano kwa Umma
MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)
PIA SOMA
- NHIF yalegeza masharti ya bima ya Toto Afya Kadi