Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
TAARIFA KWA UMMA
Kwa mujibu wa Kifungu cha 5(1) kikisomwa pamoja na jedwali la Sheria ya Shirika la Posta ya Mwaka 1993 Kipengele cha 1(1)(b) pamoja na Tamko la Waziri Na. 845 lililochapishwa kwenye Gazeti la Serikali la tarehe 15 Novemba, 2019 vinampa Mamlaka Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuteua Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Shirika. Kwa mamlaka hayo. Mheshimiwa Jerry William Silaa (Mb.) Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amemteua Bw. Toyi A. Ruvumbangu kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania na amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi hiyo:
1. Bi, Caroline D. Kanuti
2. Bi. Nura Mohamed Abubakari
3. Bw. Matimbila 1. Paul
4. CPA. Poniwoa A. Moisse
5. Bw. Hassan O. Kitenge
Aidha, uteuzi huo ni wa kipindi cha miaka mitatu (03) kuanzia tarehe 05 Novemba, 2024 hadi tarehe 04 Novemba, 2027.
PIA SOMA
- Baada ya Wenyeviti kuondolewa, Waziri Jerry Silaa avunja Bodi za TTCL, Shirika la Posta (TPC) na UCSAF