utukufu mwanjisi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2017
- 2,849
- 2,508
Shikamoo Mheshimiwa
Shikamoo Kaka
Shikamoo Kiongozi
Shikamoo Kiongozi Mtenda Haki
DHUMUNI la kukuandikia waraka huu, kwasababu wewe ni mmoja ya viongozi ambae amekuwa anawatendea sana haki watu wanaodhurumiwa au kutaka kudhurumiwa mali zao(ardhi), maana dhuruma za ardhi nyingi zinatokana na watu wenye uwezo na wengine wenye mamlaka serikalini na wengine wenye watu wa kuwalinda kutoka serikalini.
SASA ndani ya miezi miwili hii yaani mwezi May na mwezi June kuna vurugu kubwa sana zimetokea eneo la MADALE MIVUMONI, eneo ambalo lipo karibu na shule ya Atlas, eneo hilo linatambulika kuwa linamilikiwa na mama mmoja anaetambulika kwa jina la MONICA MBALE, lakini kuna mtu mwenye uwezo alijitokeza na kusema eneo lake japo hana document yoyote ile lakini amefanya ujanja wa kumtanguliza Waziri fulani ambae ni mstaafu na Waziri huyo amekuwa akitumia vyombo vya usalama (POLISI) kinyume cha sheria kufanya vurugu kwenye eneo hilo, Na tunajua kuwa wale POLISI wanaoletwa pale hawana sauti zaidi ya kufuata Amri ya ambae yupo nyuma ya haya yote sababu tumekuwa tukihoji hilo kwao.
WAZIRI mstaafu, Tajiri huyo, watu wao na Polisi wamekuwa wakiingia kwenye eneo na kuharibu miundombinu yote inayowekwa na huyo mama na wamekuwa wakileta hofu kwa wananchi wanaoishi pembezoni ya eneo hilo na kuhisi kuwa hawapo salama kwa yale yanayotokea pale.
HIVYO huyo mama akijaribu kupeleka nyaraka zake kwenye vyombo vya usalama kwa kuwaeleza kuwa wanakosea kwenda kufanya uharibifu kwenye eneo lile maana yeye ndie mmiliki wa pale amekuwa akiambiwa ilikuwa ni ODA kutoka juu.
BASI huyo mama anaomba msaada wa haraka kutoka kwako maana anaenda kudhurumiwa eneo lake na hao watu wana mpango wa kuliuza kwa mtu mwingine ili kuendelezamgogoro wa hapo.
NISAMEHE, maana utajiuliza kwanini UTUKUFU kaenda kuandika mtandaoni na wakati namba yako ninayo, hii ni kuhitaji msaada wa haraka kwa huyo mama kwa kuhofia kukuandika ujumbe wa whatsapp au sms ya kawaida unaweza usiione.
HAYA YOTE NIMEYAANDIKA HAPA NIMEYASHUHUDIA KWA MACHO YANGU, ΝΑ ΝΙΜΕPEWA VITISHO PIA KUHUSU ENEO HILO.