Waziri Jerry Slaa aingilia kati sakata la kukosekana kwa huduma za mitandao ya simu. Aiagiza TCRA kuchukua hatua

Waziri Jerry Slaa aingilia kati sakata la kukosekana kwa huduma za mitandao ya simu. Aiagiza TCRA kuchukua hatua

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Kwa siku mbili tatu hizi kumetokea changamoto kubwa ya mtandao kwenye upande wa MPESA ambapo watu wamekuwa wakipata changamoto katika kutokea na kupokea pesa kupitia mitandao ya simu.

Soma pia:

Siku ya leo, Jerry Slaa akiwa anajibu swali la Mbunge amedokeza kuwa Serikali inafahamu changamoto hiyo na kuongeza kuwa

"Mheshimiwa Naibu Spika ni kweli kumekuwa na shida, tulipata malalamiko makubwa kutoka vodacom ambao walikuwa wanaboresha mfumo wao wa billing system. Tayari nimewaelekeza TCRA kufanya tathmini ya suala lenyewe kama ni suala kweli la kiufundi au kuna uzembe kwenye leseni waliopewa wenzetu Vodacom, nimewaagiza TCRA wachukue hatua."

Kwa kauli hii ya Slaa ni kwamba kama TCRA wakigundua kuwa kulikuwa na uzembe, Waziri anaweza kuwapokonya Vodacom leseni ya ku-operate nchini? Au nimewaza kikondakta?

Jerry yuko katika wizara ya kimfumo, tofauti na ardhi alikuwa anapuyanga tu. Hapo ni kama yuko detention ya kisiasa tu. Sasa anaipiga mkwara Mpesa? Kama Kituo cha mafuta mikocheni kilimshinda
 
Hawa jamaa wanakera aisee.

Si wanyanganywe leseni.

Kwanini watoe huduma kimagumashi namna hii.
 
Hawa jamaa wanakera aisee.

Si wanyanganywe leseni.

Kwanini watoe huduma kimagumashi namna hii.
Watashitakiwa, tutapigwa faini tutalipishwa pesa! Shida ipo katika mikataba iliyoingia serikali na hawa wawekezaji. Lakin pia mifumo mibovu ya upatikanaji wa nafuu ya kisheria kwa wahanga wa kadhia hii...ukienda mahakama za ndani zinawabeba wawekezaji...rejea ile ya Kabsojr dhidi ya Vod....!
 
Hii Mitandao inawanyanyasa raia.

Huwezi ukawa unanfanya tu vile unajisikia.

Haiwezekani bila taarifa yeyote service haipatikani unakuja tu kuomba radhi with a simple statement.

Hawa tumewalea vibaya na siku si nyingi watatupandia kichwani tutakuja kutafutana.

Serikali iwe inawapiga faini kubwa kubwa ili wasirudie na waongeze ufanisi.
 
Back
Top Bottom