Waziri Kalemani: Vijiji vyote kuwa na umeme Desemba 2022 0

Waziri Kalemani: Vijiji vyote kuwa na umeme Desemba 2022 0

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani, amewataka Watumishi wa Shirika la umeme Tanzania ( TANESCO) pamoja na REA, kufanya kazi kwa kasi, kwa ubunifu na kwa usahihi ili kuhakikisha vijiji vyote nchini vimeunganishwa na umeme ifikapo mwezi Desemba mwaka 2022.

” Ni kauli mbiu ya Wizara ya Nishati, na ni kauli mbiu yangu kufanya kazi kwa kasi, kwa ubunifu na kwa usahihi na kila mtumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake anapaswa kuifahamu na kuitekeleza kauli mbiu hii” Amesema Dkt. Kalemani.


My Take:
Kwa hii kauli mbiu, na kwa maelezo ya Mh. Mwigulu juu ya hali halisi huko vijijini sidhani au nadhani Mh. Kalemani unataka kushindana na "Numbers" , Kumbuka "Numbers dont lie"
 
Hii ni habari mbaya sana kwa wale wanaostruggle eti kufuta legacy
 
Kama hutakifumua na kukiunda upya kitengo Cha surveyor nchi nzima, umeme hautakaa ufike kila mahali kijijini. Kwa sasa vijiji vingine vimewekwa umeme nusu. Wakipitisha umeme barabara moja zingine wanaachana Nazo.

Pili transformers zinazowekwa na REA ni ndogo sana sana,zina uwezo mdogo ambapo iwapo matumizi yataongezeka itabidi tanesco waingie gharama ya kuweka transformers kubwa.

Tatu, wakandarasi wanaoginga mihuri fomu za Umeme za wateja gharama ni kubwa sana Tsh 50,000 na service line ya tanesco ni Tsh 27,000. Sasa Cha kushangaza mkandarasi anapata fedha nyingi kuliko serikali kwa kugonga mhuri tu. Ninashauri fomu ya mkandarasi iwe flat rate Tsh 10,000 nchi nzima na service line iwe 27,000. Na itangazwe iwe wazi.

Nne, kuna mikoa mameneja wa tanesco mikoa wanawakataza wateja kuweka additional Meta za Umeme pale ambapo Pana meta nyingine. Tunaomba maelezo na usahihi wake.
 
Waziri wa mchongo mpaka sasa hakuna hata kijiji kimoja alichopeleka umeme
 
Back
Top Bottom