Waziri Kambole: Pambana kama Big Tarimo, usikubali Kukamatwa

BabaMia

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2024
Posts
270
Reaction score
554
Kufuatia sakata la Mfanyabiashara Deogratius Tarimo kunusurika kutekwa na watu wasiojulikana, Wakili wa kujitegemea, Jebra Kambole ameutumia ukurasa wake wa X kuukumbusha umma wa Watanzania sheria inasemaje pale wanapofuatwa kukamatwa na Polisi.

Wakili @Advocate_Jebra Kambole ameandika:-

“Usikubali kukamatwa na mtu ikiwa;
1. Kavaa kiraia
2. Gari halina No. au No za kiraia
3. Watu ambao hawajatoa vitambulisho
4. Watu wasiokwambia kosa lako na kwamba uko chini ya ulinzi.
5. Watu wasio na hati ya ukamataji!!”

“Pambana kama Big Tarimo!!” amesema.
 
Wakikuzidi nguvu niite mimi ...
 
Haya mambo yakiwa sio upande wako yanasikika kimasihara sana. Lakini ni matumizi mabaya ya Task Force ya upande wowote ule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…