Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Katika kufafanua hilo Majaliwa amesema:
Nitatembelea baadhi ya miradi ilizungumzwa hapa kwamba yamekuja mabilioni mabilioni, nitaenda kuona mabilioni hayo yalivyotumika kwenye miradi hiyo.
Lakini pia wakati wowote naweza kubadilisha ratiba nikaenda kwenye mradi wowote ule, muwe mmepanga nyie au nimepanga mimi, nitaambia madereva nataka kwenda huku nao watanyosha kwenda huko.
Tukiwa kwenye miradi hiyo tutakutana na Wananchi, moja kati ya jukumu letu kama Watumishi wa Umma ni kuwahudumia Wananchi na moja kati ya huduma ni kusikiliza matatizo yao ili tuyafanyie kazi tuondoe changamoto hizo waendelee na maisha yao. Kwahiyo nitapata nafasi ya kusikiliza wananchi wanasema nini.
Kwenye mikutano hii ya Wananchi Wakuu wa Idara wote mnatakiwa kuwa kwenye kituo hicho mimi ntakapokuwa. Wananchi wakija na Mabango mtalazimika kuyaacha, Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya usizuie bango lolote hiyo ndo forum yao ya kunieleza yaliyopo
Aidha, Majaliwa amewasisitiza Viongozi wakiona Mabango hayo ya Wananchi wayasome na kuyatafutia majibu badala ya kuyazuia.
PIA SOMA
- Waziri Mkuu Majaliwa - Tekelezeni kwa vitendo falsafa ya 4r za Rais Samia
- LIVE - Uzi Maalum wa Matukio ya Kiusalama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025