Waziri katika operesheni maalum ya ukaguzi wa utoaji wa risiti za kielektroniki Mlandege, mfanyabiashara aingia kwenye 18

Waziri katika operesheni maalum ya ukaguzi wa utoaji wa risiti za kielektroniki Mlandege, mfanyabiashara aingia kwenye 18

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Dkt Saada Mkuya Salum amesema serikali itaendelea kuwachukulia hatua wafanyabiashara ambao sio waaminifu wanaoenda kinyume na sheria za kodi kwa kukwepa kodi stahiki ya serikali

Waziri Mkuya ameeleza hayo wakati alipoongoza operesheni maalum ya ukaguzi wa utoaji wa risiti za kielektroniki katika maeneo ya Mlandege akiwa ameambatana na uongozi wa mamlaka ya Mapato Zanzibar ZRA ukiongozwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Said Athumani

Dkt Mkuya amesema serikali haitokuwa tayari kuona kodi inakwepwa na baadhi ya wafanyabiashara wachache wasio waminifu

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa ZRA Said Athumani amesema operesheni hizo zitakua endelevu katika maeneo yote ya unguja na Pemba

 
Back
Top Bottom