Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Mojawapo ya mabango ya wafanyakazi wa shirika la reli Tanzania walioko kwenye mgomo Tuesday, September 08, 2009 9:25 PM
Maneno hayo ni miongoni mwa maneno yaliyoandikwa kwenye mabango ya wafanyakazi wa shirika la reli Tanzania ambao wako kwenye mgomo wa malipo yao wakati walipokutana na Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa. Picha za mabango ya wafanyakazi hao mwisho wa habari hii. Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa alipokolewa na nyimbo na mabango ya kumkebehi wakati alipojitokeza kukutana na wafanyakazi wa shirika la reli nchini TRL ambao wanaendeleza mgomo wao wa malipo kwa siku ya sita sasa.
Waziri Kawambwa alipokelewa mabango yaliyokuwa yakisema "Kawambwa Wahindi wamekupa nini", "Hii ni serikali ya India au Tanzania", "Hatutaki siasa tunataka pesa" na bango jingine lilisema "Kupewa mshahara tarehe 38 Inauma".
Wafanyakazi wa shirika hilo la reli ambalo hivi sasa limeingia ubia na shirika la reli la India, walisema kuwa wataendelea na mgomo wao mpaka watakapolipwa pesa zao.
Waziri Kawambwa alifika kwenye mkutano na wafanayakazi hao wa TRL huku akipewa ulinzi wa hali ya juu wa askari wengi wenye silaha nzito pamoja na mbwa.
Kawambwa aliwataka wafanyakazi hao warudi kuendelea na kazi kama kawaida na huku madai mengine yakiendelea kushughulikiwa kwakuwa hali hiyo ya mgomo inawaathiri watumiaji wa huduma hiyo.
Aliwataka wafanyakazi hao kuwa wavumilivu kwa kuwa Serikali tayari imeshamuita Mkurugenzi Mtendandaji wa kampuni ya Rates, Vinay Agrawal kuzungumza nae juu ya uendeshaji mbovu wa shirika hilo na haitasita kuuvunja mkataba ukibainika kuwa umeshindwa kuboresha huduma hizo.
Alisema kuwa serikali imeshachoshwa na uendeshwaji mbovu wa shirika hilo na kwa sasa inachukua hatua za kuangalia hatua kwa hatua kuangalia mikataba ya kampuni hiyo na itakuwa tayari kuuvunja endapo watabaini kuna matatizo.
Mgomo huo umewaathiri zaidi abiria wa shirika hilo ambao wamekwama katika stesheni mbalimbali nchini pamoja na kurudishiwa nauli zao kwani nauli zao walizorushiwa hazijitoshelezi kutafuta usafiri mwingine kuendelea na safari zao.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3034674&&Cat=1