Waziri Kijaji asema zoezi la Utambuzi wa wanyama litafanyika bure

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa zoezi la Utambuzi wa wanyama sasa litafanyika bila gharama yoyote kutoka kwa wafugaji baada ya Serikali kuamua kugharamia zoezi hilo.

Mhe. Dkt. Kijaji amesema hayo wakati wa mkutano baina yake na wafugaji uliofanyika Februari 19, 2025 jijini Dodoma ambao ulilenga kuwahamasisha kuekelea kwenye kampeni yaa kitaifa ya chanjo naa Utambuzi wa Mifugo.

“Mhe. Waziri Mkuu alitoa maagizo ya kufanya tathmini ya zoezi hili na kufanyia kazi changamoto zote zilizolalamikiwa hapo awali ambapo mojawapo ilikuwa ni bei kubwa uwekaji hereni kwa mfugo na ndio maana Serikali sasa imeamua lifanyike bila gharama yoyote” Amesema Mhe. Dkt. Kijaji.

Aidha Mhe. Dkt. Kijaji amezuia ukamatwaji wa mifugo ambayo haitakuwa imefanyiwa utambuzi ambapo amewataka watalaam wa sekta ya Mifugo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa zoezi hilo huku akitoa rai kwa wafugaji kutumia fursa iliyotolewa na Serikali kutambua mifugo yao.
 
Hizo pesa zitarudishwa baada ya kiapo hapo November kwa tozo za barabara za kulipia na ushuru mpya kupitia luku (road tolls)
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa zoezi la Utambuzi wa wanyama sasa litafanyika bila gharama yoyote kutoka kwa wafugaji baada ya Serikali kuamua kugharamia zoezi hilo.

Mhe. Dkt. Kijaji amesema hayo wakati wa mkutano baina yake na wafugaji uliofanyika Februari 19, 2025 jijini Dodoma ambao ulilenga kuwahamasisha kuekelea kwenye kampeni yaa kitaifa ya chanjo naa Utambuzi wa Mifugo.

“Mhe. Waziri Mkuu alitoa maagizo ya kufanya tathmini ya zoezi hili na kufanyia kazi changamoto zote zilizolalamikiwa hapo awali ambapo mojawapo ilikuwa ni bei kubwa uwekaji hereni kwa mfugo na ndio maana Serikali sasa imeamua lifanyike bila gharama yoyote” Amesema Mhe. Dkt. Kijaji.

Aidha Mhe. Dkt. Kijaji amezuia ukamatwaji wa mifugo ambayo haitakuwa imefanyiwa utambuzi ambapo amewataka watalaam wa sekta ya Mifugo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa zoezi hilo huku akitoa rai kwa wafugaji kutumia fursa iliyotolewa na Serikali kutambua mifugo yao.
Wajiandae kujibu vizuri na kwa ukamilifu maswali ya wafugaji. Vinginevyo kazi hiyo itakuwa ni ngumu sana. e.g.( 1.) Nini lengo la kufanya Utambuzi (Identification) na mfugaji atanufaikaje na zoezi hilo? Jibu laweza kuwa: Siku ya Utambuzi ndo siku ya kutoa chanjo bure na pia itadhibiti kwa kiasi kikubwa wizi wa mifugo.
(2) Ni mifugo gani wanaolengwa katika zoezi hilo e.g. ng'ombe(CBPP) au mbuzi (CCPP) au nichanjo dhidi ya ndigana kali(ECF) kwa ng'ombe?
BTW: 3. Wataalam husika Wahakikishe vifaa vya kutolea huduma hiyo vipo vya kutosha e.g. Automatic syringes 30 - 50 cc na Tag applicators. Ushauri: Wanaweza kuweka pia kahuduma ka Motisha (bila malipo)siku ya kutoa Utambulisho e.g. kuhasi kwa kutumia burdizzo na sio rubber rings n.k. sambamba na hiyo Chanjo ya bure.
 
Back
Top Bottom