Waziri Kiongozi wa SMZ ameamua kuwa mfagiaji wa barabara katika Halmashauri ya Manispaa ya Zanzibar. Hatua yake hii imetokana na barabara katika halmashauri hiyo kukithiri wa michanga kiasi cha kushindwa kutofautisha iwapo ni za lami au la!
Aidha watafiti wa mambo ya siasa wanasema hatua hiyo ni sehemu ya mpango wake wa kujiweka karibu na wananchi wa visiwa hivyo katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, huku baadhi ya watendaji wa Manispaa wakidai ni njia yake ya kukwamisha ununuaji wa mtambo wa kisasa wa kusafisha barabara visiwani humo... Kwa maelezo zaidi cheki hapa
Hapo hakuna kununuliwa wala propaganda, Waziri Kiongozi ameamua kufagia barabara, labda ni kutokana na kupungukiwa na kazi za kufanya katika Ofisi yake. Hii si mara yake ya kwanza kuweka majukumu yake pembeni na kukimbilia kufanya kazi za manispaa ingawa manispaa hiyo haipo chini ya Ofisi yake.Watafitiwa wa mambo ya siasa wakisema na wewe kibungo kwa kutuwekea blog yako ya propaganda ni sehemu ya mkakati wako wa kugombea uwakilishi ili uchukue nafasi ya Shamsi 2010 au umenunuliwa kumchafua utapinga?
MMhm, hapana ila itakuwa ni kinyume chake, Zanzibar kama nchi itatoweka na kuwa mkoa fulani hivi.... Tatizo hana ubavu wa kusimama mbele ya Watanganyika... hivyo atakuwa akiburuzwa tu!Huyu WK ni nationalist mno. Akigombea na akapata tusahau muungano
Huyu WK ni nationalist mno. Akigombea na akapata tusahau muungano
Kibunango acha propaganda...
Kama unamjua vizuri Nahodha ni wazi utakubalia this is more that political expedience. This guy has always been simple person hata alipokuwa mwakilishi wa kawaida alikuwa na kibaskeli kake na mpanda daladala. Uteuzi wake ulimkutia njiani akikokota baiskeli.Na hii ni hulka ya kizanzibari ambayo tunaiona kwa viongozi wengi watokao huko. Hulka hii ndio asset muhimu ya wazanzibari hadi sasa inayowafanya kuaminika zaidi kuliko wanasiasa wengine nchini. Ingawa wakati mwengine huwa sababu ya kuzorota kwa mikakati ya kimaendeleo na kwa wengine kuonekana kama kujirahisisha mbele ya jamii ya enzi za "waheshimiwa"
Kwangu mimi huu ni ujumbe mkali kwa watendaji wa manispaa ya Zanzibar kuwajibika ipasavyo.
Omarilyas
WK is a down to earth man of the people. Watu wa aina yake kama alivyo RZ na MBM yaani watu wa kupelekwa pelekwa tuu ndio watadumisha Muungano kwa kuvumilia na kustahimilia ubabe wa Bara.Patakuwa hapakaliki hapo Zenj...
Kufagia kwa WK sio kuwa anataka kuwa karibu na walala hoi au kupata feeling au kutoa mfano, bali ni kuwapa taarifa kuwa hawawezi kazi na yeye ndio anayeweza kufagia barabara vizuri zaidi yao.Ni safi sana WK kufagia na kupata feeling ya kazi za walalahoi.Kuna viongozi ambao wakishachaguliwa tu kumwona kwa karibu ni kwenye gari la 4WD la kiyoyozi.
Baada ya muda anatakata kama katoka kwenye neema, wacha kibarua kiote nyasi ndo utamwaona akisalimia hata wananchi wake.
Tuwe karibu na watu, tufanye kazi zao cheo ni dhamana.
Duh.Akipigania Kib. kura ya kwanza ya kwangu. Na nitampiogia debe kamanda.Watafitiwa wa mambo ya siasa wakisema na wewe kibungo kwa kutuwekea blog yako ya propaganda ni sehemu ya mkakati wako wa kugombea uwakilishi ili uchukue nafasi ya Shamsi 2010 au umenunuliwa kumchafua utapinga?
Usipake mafuta kwa mgomgo wa chupaKibunango acha propaganda...
Kama unamjua vizuri Nahodha ni wazi utakubalia this is more that political expedience. This guy has always been simple person hata alipokuwa mwakilishi wa kawaida alikuwa na kibaskeli kake na mpanda daladala. Uteuzi wake ulimkutia njiani akikokota baiskeli.Na hii ni hulka ya kizanzibari ambayo tunaiona kwa viongozi wengi watokao huko. Hulka hii ndio asset muhimu ya wazanzibari hadi sasa inayowafanya kuaminika zaidi kuliko wanasiasa wengine nchini. Ingawa wakati mwengine huwa sababu ya kuzorota kwa mikakati ya kimaendeleo na kwa wengine kuonekana kama kujirahisisha mbele ya jamii ya enzi za "waheshimiwa"
Kwangu mimi huu ni ujumbe mkali kwa watendaji wa manispaa ya Zanzibar kuwajibika ipasavyo.
Omarilyas
Du Pasco I like the way u talk.WK is a down to earth man of the people. Watu wa aina yake kama alivyo RZ na MBM yaani watu wa kupelekwa pelekwa tuu ndio watadumisha Muungano kwa kuvumilia na kustahimilia ubabe wa Bara.
Kwa wapenda demokrasia ya kweli, alichotaka kufanya Jumbe na Dourado ndicho ZnZ inachotaka. Tuliyaona yaliyomkuta.
Dr. Gharib Bilal pia ni MZnZ wa kweli, yaliyomkuta tunayajua ndio maana kila siku Seif anashinda lakini hapewi nchi, kisa bara yaogopo Seif hata pelekwa pelekwa.
2010 kama sio Mwinyi ni Seif Khatib, lazima wabara wawapangie. Walahi WZnz wakichoka, hata wana CCM wataipa CUF, na ndipo Muungano afanyiwe mapitio kwa ZnZ kupewa haki zake stahili kama mbia mwenye haki sawa na sio mmoja kumburuza mwingine.
Kufagia kwa WK sio kuwa anataka kuwa karibu na walala hoi au kupata feeling au kutoa mfano, bali ni kuwapa taarifa kuwa hawawezi kazi na yeye ndio anayeweza kufagia barabara vizuri zaidi yao.
Hafagii barabara kama motisha kwa wafanyakazi hao, ambao wanafanya kazi hiyo katika mazingira magumu bali ni sehemu yake ya kukataa wazo la kununuliwa kwa mtambo/mashine/gari la kuweza kusafisha barabara na hivyo kuziba pengo la upungufu wa wafanyakazi katika kitengo cha wasafisha barabara wa Halmashauri ya Manispaa ya Zanzibar.
Rejea hotuba yake ya kufunga kikao cha Baraza la Wawakilishi aliyoitoa mwishoni mwa mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nahisi ujanifahamu. Kuna tatizo la muda mrefu la uchafu wa barabara, na kinachotakiwa ni uvumbuzi wa kudumu kuona kuwa barabara hizo haziwi chafu tena.Hata hivyo, Kinu it is all in the positive side kwa wananchi,viongozi wangapi wanjishusha?
Nahisi ujanifahamu. Kuna tatizo la muda mrefu la uchafu wa barabara, na kinachotakiwa ni uvumbuzi wa kudumu kuona kuwa barabara hizo haziwi chafu tena.
Sasa iwapo WK atafagia barabara ambapo hardly itakuwa chini ya nusu saa, bado hatakuwa ametatua tatizo hilo ambalo limeripotiwa katika Baraza la Wawakilishi. Anachojaribu kufanya ni sawa na kejeli kwa wafagiaji wa kila siku wa barabara hizo na sio kujishusha kama unavyodai.