Pre GE2025 Waziri Kivuli wa ACT Wazalendo Ndolezi Petro atangaza nia ya kugombea Ubunge jimbo la Kigoma Kusini

Pre GE2025 Waziri Kivuli wa ACT Wazalendo Ndolezi Petro atangaza nia ya kugombea Ubunge jimbo la Kigoma Kusini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mhandisi Ndolezi Petro, Waziri Kivuli wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Vijana, Kazi na Ajira kutoka ACT Wazalendo, ametangaza nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika uchaguzi wa 2025.

Akizungumza Januari 16, 2025, kijijini Nguruka, alisisitiza dhamira yake ya kushughulikia changamoto za jimbo hilo, ikiwemo miundombinu mibovu, ukosefu wa pembejeo za kilimo, migogoro ya ardhi, na huduma duni za afya vijijini.

Pia ameahidi kuzingatia ajira kwa vijana, kuimarisha Baraza la Taifa la Vijana, na kuhakikisha sekta isiyo rasmi inajumuishwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

ACT Wazalendo ilifungua rasmi mchakato wa watia nia kwa nafasi za uongozi Januari 15, 2025, ambapo Dorothy Semu na Othman Masoud wamejitokeza kugombea urais kwa Tanzania Bara na Zanzibar.


IMG_0188.jpeg



Source: Jambo TV
 
Back
Top Bottom