Waziri Kombo aagana na Balozi wa Iran

Waziri Kombo aagana na Balozi wa Iran

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
mini_magick20241118-4232-owxhff.jpg

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameagana na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Mhe. Hossein Alvandi Bahineh ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 15 Novemba,2024 katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, Mhe. Waziri Kombo, amempongeza Mhe. Balozi Bahineh kwa kumaliza utumishi wake nchini na kumsihi akawe Balozi mzuri wa Tanzania nchini kwao.

mini_magick20241118-4232-t6bybi.jpg

Mhe. Waziri Kombo pia amempongeza Mhe Balozi Bahineh kwa kazi nzuri ya kuimarisha uhusiano na Ushirikiano Kati ya Tanzania na Iran ambayo ameifanya katika kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini.

Amesema katika kipindi chake uhusiano Kati ya Tanzania na Iran umeendelea kuimarika na kutanua wigo wa maeneo ya ushirikiano Kati ya Tanzania na Iran.

Mhe. Waziri pia ameishukuru Iran kwa kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kibiashara, na hivyo kuongeza mapato na kukuza uchumi wa Taifa.

mini_magick20241118-4232-whq8ai.jpg

Naye Balozi wa Iran Mhe. Bahineh ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Mhe. Balozi Bahineh amesema uhusiano kati ya Iran na Tanzania uliodumu kwa miaka 42, umesaidia mataifa hayo kukuza biashara na uchumi, na kuleta maendeleo kwa watu wake.

mini_magick20241118-4232-whq8ai.jpg

Balozi Bahineh amesema kupitia uhusiano mzuri wa kibiashara kati ya Iran na Tanzania , Iran imefanikiwa kukuza mapato yake kutoka Dola milioni 23 za Marekani hadi kufikia Dola milioni 99, kutokana na kukua kwa soko la bidhaa zake nchini.

Ameipongeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kufanikisha Mkutano wa Tüme ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Iran (JPC), uliofanyika mwezi Oktoba 2024 jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kufanyika kwa mkutano huo kumewezesha wafanyabiashara wa Tanzania na Iran kufanya vikao vya kibiashara na kisekta na kusaini Hati za makubaliano ya ushirikiano kwa utekelezaji.
 

Attachments

  • mini_magick20241118-4232-9vyi07.jpg
    mini_magick20241118-4232-9vyi07.jpg
    105.6 KB · Views: 2
  • mini_magick20241118-4232-bfvq2u.jpg
    mini_magick20241118-4232-bfvq2u.jpg
    120.5 KB · Views: 2
SISI TUPO KARIAKOO NDUGU ZETU WAMEKUFA KWA UZEMBE WA SELIKALI.

SELIKALI HAINA VIFAA VYA UOKOAJI.

HAINA WATAALAMU WA KUKABILIANA NA MAJANGA.

GHOROFA NNE TU KESHO NI SIKU YA NNE ZINAWASHINDA.

WATU WANAJENGA NA KUBOMOA KIHOLELA , VIBALI NAVYO VINATOLEWA KIHOLELA.

KARIAKOO HAINA OPEN SPACE, PUBLIC TOILET, MAJI , WALA PAKING. NI UHUNI MTUPU.
 
Nyuma ya diplomasia , kumejificha ujasusi wa kutisha .
 
Back
Top Bottom