Waziri kortini kwa kupora ardhi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Waziri kortini kwa kupora ardhi


na Ambrose Wantaigwa, Tarime


WAZIRI wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka amefunguliwa kesi akidaiwa kuvamia ardhi na kusababisha uharibifu wa mali yenye thamani ya sh milioni 10. Katika kesi hiyo namba 74/2011 iliyofunguliwa katika Mahakama ya Ardhi wilayani hapa ilidaiwa na mlalamikaji, Ally Mrimi, mkazi wa Tarime mjini kuwa waziri huyo alivamia uwanja wake na kusababisha uharibifu huo.
Mlalamikaji alidai wakati uwanja wake unavamiwa kulikuwapo na mawe, mchanga pamoja na uzio.
Katika utetezi wake kupitia wakili wa Makowe Chambers Advocates, waziri huyo alikanusha madai hayo na kudai yeye ni mmiliki halali wa uwanja huo kutokana na hati iliyotolewa kisheria namba 23284 iliyotolewa Machi 28 mwaka 2009, hivyo kuiomba mahakama kutupilia mbali madai hayo.
Aidha, alidai hawezi kulipa fidia inayodaiwa na mlalamikaji kwa kuwa kisheria hakuna sababu ya mdaiwa kulipa fidia kutokana na kosa ambalo hakutenda.
"Kutokana na ukweli huo wa vielelezo ikiwa pamoja na nakala ya hati ya kumiliki ardhi iliyotolewa kisheria tunaiomba mahakama yako itupilie mbali madai hayo ikiwa ni pamoja na kulipwa gharama za kesi na mdai"� ilieleza sehemu ya hati hiyo ya utetezi.
Hoja ya kupinga madai hayo, ilieleza kuwa wakala wa Barabara TANROADS ndio wenye dhamana ya kudai eneo hilo kutokana na kuwa eneo la hifadhi ya barabara na si la mlalamikaji.
 
Kasi ya serikali ya JK kupora ardhi za raia wanyonge kweli sasa inatisha.................................
 
Utashangaa huyu waziri pamoja na kesi hii hata jiuzulu wala hata wajibishwa! Hiyo ndio nchi yetu ya wadanganyika! Uwajibikaji hakuna kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…