Pre GE2025 Waziri Lukuvi atembea ofisi za ACT Wazalendo; Asema chaguzi zitakazofanyika wakati wa utawala wa Rais Samia zitakuwa zenye heshima, huru na haki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
lukuvinyika.jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Ndg. William Lukuvi akiwa ameambatana na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mtungi leo 07/10/2024 ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya ACT Wazalendo na kupokelewa na Kiongozi wa Chama Ndg. dorothy Semu aliyeambatana na Katibu Mkuu Ndg. Ado Shaibu.

Katika mazungumzo yao, KC Dorothy Semu amemweleza Waziri Lukuvi hofu waliyonayo wananchi kuhusu chaguzi zijazo za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025 ikiwa zitakuwa huru na za haki.

Ndugu Semu amesema katika ziara ya Chama iliyofanyika katika majimbo yote nchini viongozi wameelezwa na kujionea hali ya wananchi isiyoridhisha na kwamba bado hawana imani na vyombo vya serikali katika kusimamia masuala yao ikiwemo uwepo wa uchaguzi huru na wa haki. Vilevile, watendaji wa ngazi za chini bado wanaendelea na vitisho kwa wananchi ili kuwazuia wasishiriki kutekeleza haki zao za kidemokrasia na kiraia.

Kwa upande wake, Waziri Lukuvi akitoa salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Samia Suluhu amewahakikishia viongozi wa ACT Wazalendo kuwa Rais Samia amedhamiria kuhakikisha kuwa chaguzi zote zitakazofanyika wakati wa utawala wake zitakuwa zenye heshima, huru na za haki.

Aidha, Ndugu Lukuvi amempongeza Ndugu Dorothy Semu kwa kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya ACT Wazalendo kuaminiwa na kuchaguliwa katika nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa Chama na kwamba hiyo inaonesha kiasi gani Chama kimemwamini.

Ndugu Lukuvi ametumia fursa hiyo pia kumpongeza Kiongozi wa Chama Mstaafu Ndugu Zitto kwa hatua yake ya kuachia madaraka na kutoa nafasi kwa wengine jambo ambalo limekuwa gumu kwa wanasiasa wengi.

"Nampongeza sana pia Zitto. Kwa umri mdogo alionao, na ukizingatia ndiye mwasisi wa Chama, kukubali kuachia madaraka ya uongozi, ametoa funzo kubwa. Anaonyesha ukomavu wa kutosha katika fikra zake" amesema.

Ziara ya Waziri Lukuvi katika ofisi za Makao Makuu ya Chama leo ni sehemu ya utaratibu aliojiwekea akiwa Waziri mwenye dhamana na Vyama vya Siasa kutembelea vyama hivyo na kubadilishana mawazo wakati huu nchi inapoelekea katika chaguzi.

Hapa ninapoona mapungufu ya KATIBA ya sasa. Yani Waziri wa serikali ya ccm atembelee vyama pinzani na ccm , huku yeye mwenyewe ni mbunge wa ccm....loh , ndio mana ilipaswa mawazjri wasitokane na vyama.
 
Ok ccm wanafuta chama Cha kuwasaidia kufake uchaguzi

Mwaka huu fomu za act zitapokelewa na fomu za chadema zitakataliwa
 
..Lukuvi ambaye ni kada wa Ccm hapaswi kuambatana na Msajili wa vyama kutembelea vyama vya siasa.

..badala yake Katibu Mkuu wa Wizara husika ndio aambatane na Msajili ktk ziara hiyo.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Ndg. William Lukuvi akiwa ameambatana na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mtungi leo 07/10/2024 ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya @ACT Wazalendo na kupokelewa na Kiongozi wa Chama Ndg. @dorothy Semu aliyeambatana na Katibu Mkuu Ndg. @Ado Shaibu.
Wanazungumziaje kauli ya Chalamila na yule wa Bukoba
 
Hapa ninapoona mapungufu ya KATIBA ya sasa. Yani Waziri wa serikali ya ccm atembelee vyama pinzani na ccm , huku yeye mwenyewe ni mbunge wa ccm....loh , ndio mana ilipaswa mawazjri wasitokane na vyama.

..naungana na wewe 100%.

..siku ya Lukuvi kutembelea makao makuu ya Ccm sijui itakuwaje.

..hawajalenga ku-support vyama vya siasa, bali kujisafisha kwa wanaofuatilia siasa za Tanzania.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Ndg. William Lukuvi akiwa ameambatana na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mtungi leo 07/10/2024 ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya ACT Wazalendo na kupokelewa na Kiongozi wa Chama Ndg. dorothy Semu aliyeambatana na Katibu Mkuu Ndg. Ado Shaibu.

Katika mazungumzo yao, KC Dorothy Semu amemweleza Waziri Lukuvi hofu waliyonayo wananchi kuhusu chaguzi zijazo za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025 ikiwa zitakuwa huru na za haki.

Ndugu Semu amesema katika ziara ya Chama iliyofanyika katika majimbo yote nchini viongozi wameelezwa na kujionea hali ya wananchi isiyoridhisha na kwamba bado hawana imani na vyombo vya serikali katika kusimamia masuala yao ikiwemo uwepo wa uchaguzi huru na wa haki. Vilevile, watendaji wa ngazi za chini bado wanaendelea na vitisho kwa wananchi ili kuwazuia wasishiriki kutekeleza haki zao za kidemokrasia na kiraia.

Kwa upande wake, Waziri Lukuvi akitoa salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Samia Suluhu amewahakikishia viongozi wa ACT Wazalendo kuwa Rais Samia amedhamiria kuhakikisha kuwa chaguzi zote zitakazofanyika wakati wa utawala wake zitakuwa zenye heshima, huru na za haki.

Aidha, Ndugu Lukuvi amempongeza Ndugu Dorothy Semu kwa kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya ACT Wazalendo kuaminiwa na kuchaguliwa katika nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa Chama na kwamba hiyo inaonesha kiasi gani Chama kimemwamini.

Ndugu Lukuvi ametumia fursa hiyo pia kumpongeza Kiongozi wa Chama Mstaafu Ndugu Zitto kwa hatua yake ya kuachia madaraka na kutoa nafasi kwa wengine jambo ambalo limekuwa gumu kwa wanasiasa wengi.

"Nampongeza sana pia Zitto. Kwa umri mdogo alionao, na ukizingatia ndiye mwasisi wa Chama, kukubali kuachia madaraka ya uongozi, ametoa funzo kubwa. Anaonyesha ukomavu wa kutosha katika fikra zake" amesema.

Ziara ya Waziri Lukuvi katika ofisi za Makao Makuu ya Chama leo ni sehemu ya utaratibu aliojiwekea akiwa Waziri mwenye dhamana na Vyama vya Siasa kutembelea vyama hivyo na kubadilishana mawazo wakati huu nchi inapoelekea katika chaguzi.

Kwa hivyo inategemea Rais? Akiwa mwenye imani mambo yanakuwa mazuri, akiwa asie na imani mambo huwa mabaya? Jk na sasa mama Samia
 
Hapa ninapoona mapungufu ya KATIBA ya sasa. Yani Waziri wa serikali ya ccm atembelee vyama pinzani na ccm , huku yeye mwenyewe ni mbunge wa ccm....loh , ndio mana ilipaswa mawazjri wasitokane na vyama.
Ahadi za kuwa huru na waheshima ni nzuri ila sii kwa mazingira yetu,itakuwa endapo labda ikawa yanazungumziwa mazingira ya mbinguni.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Ndg. William Lukuvi akiwa ameambatana na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mtungi leo 07/10/2024 ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya ACT Wazalendo na kupokelewa na Kiongozi wa Chama Ndg. dorothy Semu aliyeambatana na Katibu Mkuu Ndg. Ado Shaibu.

Katika mazungumzo yao, KC Dorothy Semu amemweleza Waziri Lukuvi hofu waliyonayo wananchi kuhusu chaguzi zijazo za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025 ikiwa zitakuwa huru na za haki.

Ndugu Semu amesema katika ziara ya Chama iliyofanyika katika majimbo yote nchini viongozi wameelezwa na kujionea hali ya wananchi isiyoridhisha na kwamba bado hawana imani na vyombo vya serikali katika kusimamia masuala yao ikiwemo uwepo wa uchaguzi huru na wa haki. Vilevile, watendaji wa ngazi za chini bado wanaendelea na vitisho kwa wananchi ili kuwazuia wasishiriki kutekeleza haki zao za kidemokrasia na kiraia.

Kwa upande wake, Waziri Lukuvi akitoa salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Samia Suluhu amewahakikishia viongozi wa ACT Wazalendo kuwa Rais Samia amedhamiria kuhakikisha kuwa chaguzi zote zitakazofanyika wakati wa utawala wake zitakuwa zenye heshima, huru na za haki.

Aidha, Ndugu Lukuvi amempongeza Ndugu Dorothy Semu kwa kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya ACT Wazalendo kuaminiwa na kuchaguliwa katika nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa Chama na kwamba hiyo inaonesha kiasi gani Chama kimemwamini.

Ndugu Lukuvi ametumia fursa hiyo pia kumpongeza Kiongozi wa Chama Mstaafu Ndugu Zitto kwa hatua yake ya kuachia madaraka na kutoa nafasi kwa wengine jambo ambalo limekuwa gumu kwa wanasiasa wengi.

"Nampongeza sana pia Zitto. Kwa umri mdogo alionao, na ukizingatia ndiye mwasisi wa Chama, kukubali kuachia madaraka ya uongozi, ametoa funzo kubwa. Anaonyesha ukomavu wa kutosha katika fikra zake" amesema.

Ziara ya Waziri Lukuvi katika ofisi za Makao Makuu ya Chama leo ni sehemu ya utaratibu aliojiwekea akiwa Waziri mwenye dhamana na Vyama vya Siasa kutembelea vyama hivyo na kubadilishana mawazo wakati huu nchi inapoelekea katika chaguzi.

CCM kuendelea kubaki madarakani au kushinda uchaguzi wa siasa hapa Tanzania haitegemei kupigiwa kura na mtu yoyote yule.
 
Back
Top Bottom