Waziri Lukuvi, sio lazima kisheria jina la mke na mme kuwa kwenye hati ya kiwanja

Waziri Lukuvi, sio lazima kisheria jina la mke na mme kuwa kwenye hati ya kiwanja

Bashir Yakub

Member
Joined
May 27, 2013
Posts
96
Reaction score
1,745
NDG. LUKUVI, SIO LAZIMA KISHERIA JINA LA MKE NA MME KUWA KWENYE HATI YA KIWANJA.

Na Bashir Yakub, WAKILI
+255 714 047 241.

Lazima tunapotoa kauli tuwe tunatofautisha matamanio yetu, na kile sheria inachosema. Tuangalie haya 6 kuhusu kauli ya ndg Lukuvi.

1. Mpaka sasa hakuna sheria inayolazimisha kuwa jina la mke na mme lazima yawe kwenye hati ya kiwanja. Tuna Sheria ya Ardhi Na. 4, Na.5, Sheria ya Usajili wa Ardhi Sura ya 334, Sheria Na. 17/2008 ya Rehani ya Mikopo nk nk.

Zote hizi hakuna jambo hilo, isipokuwa limefanywa kuwa la hiari.

2. Tafsiri ya neno Umiliki wa Ardhi, ni umiliki unaohusu mtu mmoja peke(exclusively), mtu zaidi ya mmoja(co-occupancy), ushirika(partnership), kampuni nk. Soma kifungu cha 19(1) cha Sheria ya ardhi Na.4.

Kwa mujib wa kifungu hiki umiliki wa mtu mmoja peke haujafa bado upo.

3. Kwà mujib wa Sheria ya Ndoa ili mwanandoa awe na share kwenye kiwanja/mali lazima awe amechangia(joint effort/contribution). Hata km alifanya kaz za ndan(domestic duties) ni mchango, la msingi lazima achangie.

4. Si lazima hati ya kiwanja iwe na majina yote ya mke na mme ndipo haki ya umiliki wa pamoja ipatikane. Hati inaweza kuwa na jina la mmoja mf. mme tu lakini mke bado akawa na haki/share.

Haki ya pamoja inatokana na nguvu/jitihada za pamoja(joint efforts) ktk upatikanaji wa mali husika, haitokani na nani kaandikwa kwenye hati.

5. Sheria ya Ardhi na ya ndoa zinahuruhusu kitu kinaitwa "ESTATE PLANNING" . Kupitia hiki kitu wanandoa wanaweza kuamua baadhi ya mali ziwe zao wote yaani za ndoa, na baadhi kila moja imilikiwe na mmoja bila kumhusisha mwingine.

Kitu hiki kinaweza fanyika kabla ya ndoa km maandalizi ya ki-mali ya kuingia kwenye ndoa ili kuepusha mgogoro baadae, au ndani ya ndoa tayar.

Kupitia kitu hiki ndipo wanandoa wanaweza amua kusajili ardhi kwa majina yao wote wawili ama hapana.

6. Lukuvi anaongelea ardhi zenye hati, vipi zile ambazo hazina hati anatwambiaje. Kuwa wakienda kuandikishana huko serikali za mitaa wanakoendaga(japo hairuhusiwi) wawabebe na wake zao au waume zao ndo mauziano ya ardhi yawe halali !!!.

Atangaze bas taifa zima lijue kuwa kuanzia sasa ni kosa kisheria kununua ardhi bila mke au mme wako.

Pia soma
 
Kuna mgongano wa tafsiri ya sheria ambao mpaka sasa hakuna uamuzi wa mahakama ulioutatua ;

Kwa maana kwamba sheria ya ndoa inatambua machumo ya ndoa (matrimonial property)

Lakini wakati huo huo inatambua haki ya mwanandoa kuwa na mali yake binafsi.

Sheria ya ndoa haitamki kwamba mali lazima ziwe na majina ya wanandoa,

Ila case law inatambua mchango wa mwanandoa katika upatikanaji wa machumo ya ndoa.

Hivyo kauli ya Waziri haina nguvu yeyote ile kisheria.
 
Hili liambatane na elimu ya ndoa, sheria ya ndoa na mbadala wa kubadili maamuzi uwepo.

Sio ajabu mwanamke akaingia kwenye ndoa ili tu aje kupata kiwanja,.mana kwa sasa kiwanja imekuwa mali kubwa kuliko hata gari kwa wenye akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani Mungu ni mkubwa na kitu bahati hakika kipo. Yaani huyu mzee anasifiwatu lakini kero za ardhi kwenye miji,manispaa na majiji bado zipo lukuki na zinasababishwa na watendaji wa ardhi wakipewa nguvu na baadhi ya wakurugenzi.

Ninadhani wanaosababisha migogoro hiyo wananufaika nayo.

Ninawiwa kusema Lukuvi asaidiwe nguvu zimepungua hawezi kushurutisha wazembe.
 
Kwani nani kasema kisheria ni lazima Hati iwe na jina la mkeo?
 
Kwani nani kasema kisheria ni lazima Hati iwe na jina la mkeo?

Inaelekea hujasoma taarifa nzima ya mleta mada...

Aliyesema ni William Lukuvi, Waziri wa Ardhi...

Kasema, "....kuanzia sasa hati za umiliki wa ardhi lazima ziwe na majina ya mume na mke..."

Maana yake ni kuwa, kama hujaolewa na unataka kumiliki ardhi, basi, sharti utafute mume kwanza akuoe ndipo utakuwa na haki ya mtapata hati ya umiliki ardhi itakayotolewa kwa majina yenu wote wawili..!!
 
Hili jambo ni zuri sana kufanyika maana hapo awali kwa mifumo dume iliyokuwepo kila kitu kilikuwa kinaandikwa jina la Mwanaume hata kama zaidi ya 80% ya fedha katoa mwanamke!
Halafu ndugu wa mume wanakuja juu kusema vya ndugu yao!
 
Umekosea. Hakusema hivyo. Yeye amesema kuwa kuna uwezekano wa hati kuandikwa majina ya mke na mme na akatoa wito kwa watu kuitumia fursa hiyo.

Kama kasema hivyo, tunabishania nini sasa hapa?

Ina maana hata mwanasheria Yakubu aliyeposti mada hii hakumwelewa Waziri Lukuvi siyo?

Utaratibu ndivyo ulivyo siku zote. Hati zingine za umiliki ardhi wala siyo lazima ziwe na majina ya mume au mke...

Hati ya umiliki ardhi inaweza kuwa hata na majina ya watoto ama mtu yeyote unayependa awe kwenye hati hiyo...
 
Mmnh?!
Aisee sizani kama ni hivyo ulivyomalizia!
Nafikiri hati yaweza kuwa na jina moja au mawili kumtegemeana kama mmechanga ktk kuinunua au mmekubaliana wenyewe au mke au mume peke yake!

Yes, ndivyo ilivyo siku zote...

Nadhani wanaoanzisha mada, wanaitafsiri vibaya kauli ya waziri au wanakuwa wamesikia toka kwa mtu wa tatu na kuibeba hivyo hivyo...

Kwa kifupi waziri katoa ushauri tu kwa wanaotaka kumiliki ardhi kisheria wala hajalazimisha wala kutunga sheria nyingine...
 
Kama kasema hivyo, tunabishania nini sasa hapa?

Ina maana hata mwanasheria Yakubu aliyeposti mada hii hakumwelewa Waziri Lukuvi siyo?

Utaratibu ndivyo ulivyo siku zote. Hati zingine za umiliki ardhi wala siyo lazima ziwe na majina ya mume au mke...

Hati ya umiliki ardhi inaweza kuwa hata na majina ya watoto ama mtu yeyote unayependa awe kwenye hati hiyo...
HII HAPA HABARI.

Serikali imesema sheria inaruhusu hati ya kumiliki viwanja kuandikwa majina ya familia ikiwemo mume, mke pamoja na watoto hatua ambayo itasaidia kuondoa migogoro ya mirathi.

Akizungumza leo Jumamosi Desemba 19, mkoani Kilimanjaro. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliamu Lukuvi amesema kwa sasa wizara hiyo inasajili majina hayo na kwamba Watanzania watumie fursa hiyo vema kupunguza migogoro ya mirathi.

“Sisi katika wizara hii na serikalini humu tunapata shida sana ya kushughulikia mambo ya mirathi,wizara inakubali kusajili hati kwa majina zaidi ya mawili hata ukita baba,mama na watoto kusajili hati Moja inaruhusiwa hii inasaidia kuepusha matatizo ya miradhi hapo baadae,” amesema Lukuvi.

Aidha, Waziri Lukuvi ametoa wito kwa Watanzania wote kuona umuhimu wa kufanya hivyo kutokana na kwamba keai nyingi za miradhi huwa na changamoto nyingi”alisema

“Kesi nyingi za mirathi wanakuja wajomba ambao hawakujua jasho lenu ambalo mmelichuma wanaandika hati wao wanajimilikisha hiyo ni fursa kwa wananwake…washawishini waume zenu wakati wa kuandika hati mje na majina yenu wote…hata kama umeoa wanawake watatu, sheria ipo wazi,ukija na jina la mtoto chini ya miaka 18 tutasajili jina lake na msimamizi wake.

“Ndoa zote tutaandikisha, akifa mke mmoja inafahamika kwamba haki iliyobaki ni ya wake wawili waliobaki na kwa upande wa mtoto akifikisha miaka 18 kunauwezekano wa kufuta majina ya awali ya wazazi na kumuachi mtoto,” amesema Lukuvi.

Aidha amesema utaratibu huo ikifiatwa hakutakuwa na vikao vya familia vya miradhi na migogoro isiyo ya lazima.

“Sio lazima kwamba mtu alitaka hati aje na mme wake zao Ila ni jukumu langu kuwalemisha kwamba Hilo linawezek,” amesema.

Mtanzania
 
Hili jambo ni zuri sana kufanyika maana hapo awali kwa mifumo dume iliyokuwepo kila kitu kilikuwa kinaandikwa jina la Mwanaume hata kama zaidi ya 80% ya fedha katoa mwanamke!
Halafu ndugu wa mume wanakuja juu kusema vya ndugu yao!
Kwa upande mmoja waweza ona lina manufaa sana lkn kwa upande wa pili linawatia vijana hofu ya kuoa kama itakua ni lazima jambo litakalofanya masingo mama kuongezeka kwa wanaume kukana mimba kwa hofu ya kutotaka kuishi na mwanamke.
 
Back
Top Bottom