Waziri ''Maestro'' na Little Stevie Wonder

Waziri ''Maestro'' na Little Stevie Wonder

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
WAZIRI ''MAESTRO'' ALLY NA LITTLE STEVIE WONDER

Watafiti wote naamini haweshi kujuta wanapomaliza kumhoji mtu kisha mtu yule akawa hapatikani tena kwa sababu yoyote ile kwa kujilaumu kwa nini sikumuuliza hiki au kile.

Nimepata picha ya Waziri naamini ya miaka ya katikati 1960s akiwa na Lucky Star ya Shakila Tanga akipiga organ.

Najilaumu kwa nini muda wote katika miaka yote niliyokuwa na Maestro sikukaa na yeye kitako tukazungumza utoto wake Tanga alipoanza muziki na kumpigia Shakila wa Lucky Star.

Inaelekea Maestro alianza muziki kipindi kile kile ambacho Stevie Wonder alianza Marekani kwa kurekodi na Tamla Motown ya Berry Gordy.

Shakila halikadhalika alikuwa akirekodi muziki wake na kutoa santuri huku kwetu na bila shaka sauti yake ikisindikizwa na na kinanda cha Waziri Ally.

Lakini wapi tutapata ''discography,'' ya Shakila na Lucky Star na kusikiliza keyboard ya Maestro?
Labda Masoud Masoud Manju la Muziki anaweza kutusaidia.

Leo nimezungumza na jamaa zangu Tanga kutafuta habari za Waziri akiwa na Shakila na Lucky Star.
Naambiwa Lucky Star takriban wote wametangulia mbele ya haki hawa ndiyo wangeliweza kunipa historia ya enzi zile.

Lakini sijakata tamaa.
Afrika tuna shida zetu nyingi tu.

Nimemtafuta Stevie Wonder.

Taarifa zake zote zipo kiasi inaweza kukuzamisha ukapotea baharini kwa uzito wake.

Huyo kulia ni Stevie Wonder ambae kama nilivyosema hapo juu alianza muziki wakati mmoja na Maestro na wote wakiwa wapiga kinanda wa sifa.

WAZIRI NA STEVIE.jpg
 
Umenikumbusha vionjo vya zamani hapa nasikiliza the manhattan na kibao chao kiss and say goodbye huku sauti nzito ya wilfred "blue "Lovett ikiburudisha penye intro ni burdani
 
Picha Kwa hisani kubwa ya mdau wa muziki Muhidin Issa Michuzi blog :

Waziri Ally (nyuma kushoto) na kundi zima la Lucy Stars enzi hizo bado anasoma huko Tanga.
N.B
Mzee Mohamed Said utafiti wako ukiwatafuta wakongwe wa masuala ya muziki ikiwemo ma born-town wakongwe unaweza kukamilisha utafiti wa maisha ya Waziri Ally Maestro. Kama kijana ninapenda kufuatilia simulizi zako nyingi za historia n.k nikatoa ushauri zama hizi za kidijitali iwe unataka kuandika kitabu kuhusu nguli fulani tumia zana / tools zote za teknolijia katika hatua ya mwanzo kuhifadhi matayarisho ya kazi zako mapema kwa kutumia digital video camera pamoja na voice recorder ili kuweka mazingira ya kukamilisha kazi zako kwani huyo muhusika mkuu unayetaka kumuandika ktk kitabu au historia anaweza baadaye kuingia uvivu, kuhama mji au nchi pia kukosa munkari wa kukaa chini nawe siku za baadaye muikamilishe kazi. Fursa hupatikana mwanzo kabisa.
 

Kwa hisani kubwa ya uncle John F. Kitime JFK.​

Taarab ya Tanga​

Katika miaka ya 50 wanawake tisa wa Tanga walijikusanya na kuanzisha wakaanzisha kikundi cha kuimba walichokiita Raha til Fuad maana yake Raha ya Moyo.

Akina mama hawa chini ya bibie aliyeitwa Mama Akida au aka Mama Lodi, waliendesha kikundi chao wakiwa wanaimba nyimbo za Siti Binti Sadi na tungo zao ambazo waliimba katika melody ya nyimbo za kihindi zilizotamba wakati huo.

Kundi hili liliendelea na kuanza kuruhusu wanaume kujiunga hasa wakiwa wapiga vyombo. Hata mtoto wa Mama Akida, Akida Jumbe hatimaye alijiunga na kundi hili kama mpiga accordion kwenye mwaka 1962.

Kundi hili ambalo baadae lilikuja kuitwa Young Noverty,liliendelea mpaka kukaweko na mgawanyiko uliozaa kundi la Shaabab Al Waatan. Hapa ndipo kukaanza mtindo wa kuweko kundi pinzani jambo ambalo kwa njia ya ajabu sana limekuwa linadumu kiasi cha miaka kumi kumi.

Miaka ya 1960s Young Noverty na Shabaab al Waatan, 1970s Lucky Star Musical Club na Black Star Musical Club, 1980 Golden Star Taarab na White Star Taarab, 1990, Babloom Modern Taarab na Freedom Modern Taarab.

Taarab ya Tanga ndo haswa inastahili kuitwa modern Taarab, kwani wao hawkufuata taarab ile iliyoletwa Zanzibar enzi ya Sultan Seyyid Barghash, kundi la taarab hii lilikuwa dogo na vyombo vyake vilikuwa pamoja na Gitaa la besi, gitaa la solo, drums bongos ,akodion au kinanda. Nyimbo zao zilikuwa fupi na si ndefu kama za Kizanzibari., nyimbo zilitegemea mipigo ya ngoma za asili za kumbwaya na chakacha na hata baadaye mitindo kama rumba,bossa nova ilitumika kama mapigo.

Na Taarab ya Tanga ndio iliyoanzisha moto wa vikundi vya taarab Tanzania Bara. Moshi kulikuwa na New Alwatan, AzimioTaarab, na Blue Star Taarab , Arusha-Blue Star Taarab, Dodoma-Dodoma Stars, Kondoa –Blue Stars, Mbeya-Magereza Kiwira, Mwanza-ujamaa Taarab, Bukoba –Bukoba Stars, na muendelezo huu uliingia mpaka Burundi kutokana na mwana muziki mmoja alie julikana kama Athmani Mkongo, alitoka Burundi na bendi yake kufika Tanga akawa mwanamuziki mahiri wa Taarab na hata kuipeleka kwao Burundi.

1627303844017.png

(Pichani Waziri Ally wa Kilimanjaro Band, wakati huo akiwa Lucky Star akipiga kinanda)

Source : Taarab ya Tanga
 
Picha Kwa hisani kubwa ya mdau wa muziki Muhidin Issa Michuzi blog :

Waziri Ally (nyuma kushoto) na kundi zima la Lucy Stars enzi hizo bado anasoma huko Tanga.
N.B
Bagamoyo,
Ahsante sana.

Ingia mohamedsaidsalum.blogspot.com.
 
Back
Top Bottom