Waziri Maghembe anastahili pongezi katika kuteua Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa

matengo

Member
Joined
Jun 1, 2011
Posts
30
Reaction score
4
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya kahawa Bw. Adolph Kumburu amekuwa akipambana kwa kutumia waadishi wa habari mbali mbali kuzuia kikao cha Bodi kinachotakiwa kufanyika tarehe 21[SUP]st[/SUP] November, 2012 kisifanyike. Kwanza kwa kumtumia Bw. Daniel Mjema mwandishi wa gazeti la Mwananchi kwenye toleo la tarehe 7[SUP]th[/SUP] November 2012 na sasa kupitia kwa mwandishi mwingine Bw. Stanley Lyamuya (Wote wa Moshi) kupitia gazeti la The African toleo la tarehe 14[SUP]th [/SUP]November 2012 kuzuia kikao cha Bodi kisifanyike.

Anajaribu kutumia tamko la Mheshimiwa Waziri Mkuu aliposema hatma ya Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa inasubiri maamuzi ya Rais. Hata hivyo anajidanganya kwa vile Mheshimiwa Waziri Mkuu hakuvunja Bodi na wala hakuna anayejua kama mh. Rais atavunja Bodi. Hivyo Bodi iko kihalali kwa mujibu wa sheria na inatakiwa kuendelea kutekeleza majukumu yake. Kinachomfanya apambane kuzuia kikao cha Bodi kisiwepo ni kutokana na kutapatapa asijue cha kufanya wakati huu anapoandaa Board paper na hasa katika kipengele cha Yatokanayo kwa vile maagizo yote aliyopewa katika kikao cha Bodi kilichotangulia aliyakaidi.


Bw. Kumburu kupitia waandishi wa habari anasambaza uongo ili ionekane Bodi ya Wakurugenzi iliyopo haikuteuliwa kisheria. Uongo huo ni vizuri ukakanushwa kwa vile kama alivyosema mheshimiwa Rais, uongo ukiachiwa urudiwe mara nyingi bila ya kutokea wa kuukanusha basi inaweza ikafikia mahala watu wakaanza kuuamini.


Sheria ya kahawa ya mwaka 2001 kifungu Na. 35(1) kinampa madaraka Waziri wa Kilimo kutunga kanuni za kahawa. Na katika hili sheria haimbani waziri kushirikisha wadau katika kutunga kanuni. Kwa maana hiyo, siyo lazima kisheria kufuata kila maoni yatakayotolewa na wadau. Kwa misingi hii Waziri hakukiuka sheria yoyote katika kutunga kanuni kwani alitumia mamlaka aliyopewa kisheria kuhakikisha analinda maslahi ya wadau wote baada ya kupata maoni toka pande mbali mbali.


Aidha Waziri katika sheria hiyo hiyo ya Kahawa ya mwaka 2001 kwenye Schedule inayohusu Constitution, functions and proceedings of the Board kwenye kipengele Na. 3 cha constitution of the Board of Directors, Waziri amepewa madaraka kisheria kutazama upya uwakilishi wa wajumbe wa Bodi kutoka Taasisi mbali mbali. Nanukuhu "The minister may from time to time review the representation of the Board members from various institutions". Hii maana yake ni kwamba pamoja na uwakilishi wa wajumbe waliotamkwa kwenye sheria bado Waziri kisheria amepewa madaraka ya kurekebisha uwakilishi wa wajumbe kwa maslahi ya sekta ya kahawa.

Kwa mantiki hii nadhani uteuzi wa Bw. Hythinta kwa mfano, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa mfuko wa maendeleo ya zao la kahawa ilibidi amuongeze hata kama hayuko kwenye kanuni kwa kutumia madaraka aliyopewa kisheria kwenye kifungu tajwa hapo juu ili kukidhi matakwa yaliyojitokeza. Wajumbe wengine waliwakilisha kanda kama sheria inavyotaka.


Kuhusu uteuzi wa wajumbe toka taasisi mbali mbali, ikitokea kwa bahati mbaya au nzuri wakawa wanatokea mkoa mmoja, Waziri asingeweza kuwaacha kwa vile wawakilishi wengine tayari wanatoka pamoja. Mathalani haingii akilini kama Waziri angeweza kumwacha professor Teri Mkurugenzi wa Taasisi nyeti ya TaCRI kwa misingi ya kwamba hata Mh. Rais naye ametokea akamteua Mwenyekiti toka mkoa wa Kilimanjaro. Endapo angefanya hivyo hapo ndipo angekuwa anaendekeza ukabila kwa kuengua watu kwa kigezo cha ukabila.

Hivyo inabidi kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Proffessor Jumanne Maghembe kwa kuteua Bodi iliyolenga kutatua matatizo yanayosababishwa na Kumburu. Bodi yenye uwezo wa kumsimamia Mkurugenzi Mkuu kuhakikisha anaendesha shirika la umma kwa kufuata Sheria Kanuni na Taratibu zilizowekwa na Serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…