tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Kuna kila dalili kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amekalia kuti kavu, tena kavu kwelikweli.
Sakata la kuuzwa kwa faru John na kisha yeye kubariki uuzwaji huo ni udhaifu mkubwa sana na kigezo tosha cha kumfanya aondolewe kwenye nafasi yake ya sasa. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa, inasemekana faru huyo aliuzwa kwa thamani ya Tsh milion 200, ambapo wauzaji walitanguliziwa malipo ya Tsh milioni 100. Waziri mkuu hawezi kusema uongo. Ni dhahiri anazo taarifa za uhakika za kiintelejensia kwamba faru ameuzwa kwa bei hiyo ya kutupwa. Ndio maana wahifadhi wanashindwa kuonyesha kaburi lake lilipo kama kweli mnyama huyo wa porini alikufa.
Sintofahamu hii inakolezwa zaidi na Maghembe mwenyewe aliyediriki kumdanganya Waziri Mkuu, kwa kushirikiana na wezi wenzake, kwamba faru yule 'amekufa' huku akijua kwamba anasema uongo. Kwa sababu hizi, pamoja na sababu nyingine ambazo bado hazijawekwa wazi ili kumtumzia heshima profesa huyu, kuna kila dalili kwamba huenda Rais, Dr Joseph Pombe akatengua uteuzi wake kabla hajamaliza faru wetu.
Ikiwa waziri mwenye dhamana ya kulinda rasilimali zetu, ama kwa kujua au kwa makusudi, ameamua kushirikiana na majangili kufilisi rasilimali zetu kuna haja gani ya kuendelea kukalia kiti cha uwaziri? Kwa dhati kabisa bila unafiki wowote, mimi namuunga mkono Rais Pombe katika utumbuaji huu. Ifike wakati kila mtu aheshimu rasilimali za taifa kwa manufaa ya watanzania wa sasa na vizazi vijavyo.
Mungu mbariki Rais wetu, Mungu wabariki watanzania, Mungu bariki rasilimali zetu za Taifa. Amen.
[HASHTAG]#bringbackourrhinoalive[/HASHTAG]