Waziri Makamba: Umeme utaendelea kukatika mpaka tumalize maboresho. TPSF wamshukia kama mwewe

Toeni data sio planned and registered projects, hizo ni projects ambazo Zina tarajiwa hakuna investment hapo ambayo ni tayari Ina utilize umeme, leta data zinazoonyesha kuwa mwaka 2021 -2022 Kuna viwanda 50 vimejengwa na tayari vinafanya kazi , na hivi vyote vimeunganishwa katika grid ya taifa hivyo kiwango Cha umeme nchini kime pungua kulibgana na ongezeko kubwa la matumizi ya umeme, data nyingine ieleze kuwa mwaka 2020 kiasi cha umeme jumla ni 1700w Kwa watumiaji kazaa na viwanda kazaa, house hold kazaa, mwaka 2021-2022, total elecity capacity tuliyonayo ni 1700w au imeongezeka ni sawa, watumiaji wame o gezeka kuwa kiasi fulani, viwanda Vimeo ongezeka kazaa vinavofanya kazi na kutumia umeme wa taifa, maana unaweza kuwa na kiwanda kimejengwa na kina tumia umeme wake binafsi, Kwa hiyo kulingana na ongezeko hili mitambo yetu uwezo wake awali ni huu na sasa hatuwezi kukidhi matakwa ya wananchi Kwa sasa, magazette sio data, ni upuuzi kuleta taarifa za matarajio ambacho Bado hakipo katika uzalishaji.

Mbaya zaidi ni kudanganya umma kuwa mitambo ilikuwa ikifanya kazi bila maintenance Kwa miaka 6, hili ni tango pori la karne, nafikiri ni mtoto mdogo tu ndo anaweza kusikiliza story hiyo, maana hakuna mtambo unaweza ukafanya kazi miaka 6 bila repair.
 
Hivi waziri akitumbuliwa na uchapakazi wake unatumbuliwa au unabaki? Naamini professor Mhongo alikuwa na mpango kazi nina maana mambo yalikuwa nafuu tena alikuwa anatoa takwimu
 
"transfer" ndio nini?
 
Waziri Janja janja yaani mtu kuunganishiwa huo umeme tu ni shida kuna watu wanalalama wamelipia huo umeme wao tangu mwaka jana novemba hadi leo hamna kitu , nadhani afadhali hata yule kalamaini wa kule chattle aliweza hata kuwakoromea hao jamaa, huyu mkunja mikono ya shati hamna kitu kabisa , nguzo ndio usiseme zimekua dhahabu wakati miti kibao imejaa Iringa huko na maviwanda ya nguzo za zege kibaaao hayana pakupeleka mzigo.
 
Pamoja na mipango mibovu ya awali amesema pesa za matengenezo zinazohitajika ni til.4 na wamepata bil.400 tuu ndio msingi wa kwamba haijulikani umeme utaacha lini kukatika.

Kwa hiyo wewe unadhani shida ni nini kama.sio pesa za kufanyia matengenezo?
Ndugu, nikusisitizie tena ili uelewe

Tatizo la umeme wa Tanzania hii chini ya CCM haijawahi kuwa pesa!

Nimekueleza hapo mwanzo kuwa, tatizo liko tangu kuanzia kwa serikali ya awamu ya 3 chini ya Rais Hayati Ben Mkapa na kwa miaka 10 sababu zilikuwa hizi hizi zinazotolewa na kina Makamba sasa

Akaja Kikwete wa awamu ya nne, sababu zikawa hizi hizi na kwa miaka yake 10 hakuweza kulitatua tatizo la umeme pamoja na ahadi na kujipiga kifua kuwa tatizo la umeme linakwenda kuwa historia!

Tena huyu Kikwete wa CCM alianzisha project kubwa ya bomba la gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme toka Mtwara wenye thamani ya mabilioni ya shilingi. Cha ajabu project iliishia njiani. Ripoti zinasema kuwa, bomba hilo linatumika chini ya 5% kuzalisha umeme!

Akaja John P. Magufuli, akautelekeza mradi huo, naye akaanzisha wa kwake huu unaoitwa MJKN - Stigler Gorge nao una thamani ya mabilioni ya dola

Kafa Magufuli na kila kitu chake kinaelekea kufa. Yupo huyu mama na Makamba wake nao wanaimba kitu kingine kabisa!

Tatizo la nchi hii siyo PESA ndugu. Tatizo la nchi ni SERA mbovu ya nishati ya Chama Cha Mapinduzi - CCM

Ukiwa na sera mbaya, itazaliwa mipango mibaya yenye utekelezaji mbaya usio consistent. Hili ndilo tatizo Tulilo nalo hapa Tanzania

Ndiyo maana nilikuambia, HUWEZI KUTATUA TATIZO KWA KUWATUMIA WATU WALEWALE WALIOLISABABISHA TATIZO HILO....!!

CCM has to go...
 
Hapo ujue tunatakiwa tufunge mikanda sawasawa !! Bei ya bidhaa nyingi zitapanda sana na kigezo kitakuwa ni gharama za uzalishaji kupanda !!
 
Tusidanganyane hii yote ni kwa sababu ya PESA tu !!
 
Heri msema ukweli mmoja kuliko waongo 20 Tuambizane ukweli ndugu zangu

maneno ya kupeana peana moyo wakati uhalisia si kweli huwa si mazuri,Tukubali Ukweli

na tujiandae kukabiliana na hiyo changamoto, Ukweli siku zote unauma lakini ni Dawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…