Waziri Masauni amaliza mgogoro wa Jeshi na Wananchi Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani

Waziri Masauni amaliza mgogoro wa Jeshi na Wananchi Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ametatua mgogoro kati ya Jeshi la Magereza na Wananchi wa Kijiji cha Dondwe wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani baada ya wananchi hao kuzuiwa kutumia barabara inayopita katika Kambi ya Mvuti ambapo malori yanayobeba mchanga hutumia njia hiyo kwenda kubeba mchanga wa ujenzi ambao pia unatajwa kuiingizia Halmashauri mapato.

WAZIRI Masauni ametoa ruhusa ya Barabara hiyo kutumika na wananchi kuanzia saa kumi na mbili asubuh mpaka saa kumi na mbili jioni huku akitoa muda wa ruhusa hiyo kuwa ni muda wa miezi 6 huku ikisubiriwa barabara mpya iliyotolewa na Jeshi la Magereza kukamilika.
 
Majeshi yote yana la . Jwtz ni jeshi la wananchi wa Tanzania. Mshaanza kulipa ukubwa jwtz
Usichokijua wewe ni kwamba ile force unayoiona kwenye jina ni mamlaka ya kiutendaji yenye mipaka sio jina la chombo na kwa tafsiri ya kiswahili yenye kasoro ndio inatafsiriwa kama jeshi lakini wala sio chombo na haitakiwi kutamkwa "jeshi" tu bila kusema "jeshi la" hata kama tafsiri yake sio sahihi kwa sababu force sio chombo kama heading inavyomaanisha.

JWTZ linaitwa jeshi sio kwa sababu ya neno "Forces" bali ni kwa sababu chombo chenyewe kinaitwa "Military" neno lenye maana ya "Jeshi" kama chombo sio mamlaka ya kisheria. Hilo neno force(s) ni lugha ya kiraia tu na sio jina la chombo. Ndani ya jeshi lugha inayotumika ni military tu na ndio hufanya "Jeshi" kuitwa "Jeshi" bila kuongeza neno lolote.

Vyombo vyote chini ya wizara ya mambo ya ndani ni vya kiraia sio kijeshi(non military). Kule kwenye page ya Instagram ya polisi kuna post inamtaja CDF kama mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wakati ni ulinzi pekee. Sasa kama kuna hata polisi hawajui kwamba jeshi ni chombo cha ulinzi na sio usalama haishangazi hata wewe kutojua hilo.
 
NImekuja mbio nikijua ni JWTZ kumbe ni hawa walinda wahalifu wa ndani? Acha mambo yako hao walinda wahalifu sio Jeshi
 
NImekuja mbio nikijua ni JWTZ kumbe ni hawa walinda wahalifu wa ndani? Acha mambo yako hao walinda wahalifu sio Jeshi
Sahihi kabisa. Heading ina makosa. Neno Jeshi likiandikwa lenyewe moja kwa moja humaanisha Jeshi au Military kwa kiingereza na kwa Tanzania ni JWTZ.

Inabidi wanahabari na wanasiasa wapewe shule ya uraia.
 
Back
Top Bottom