TheMaster
Member
- Aug 10, 2023
- 36
- 68
Mheshimiwa Hamad Yusuph Masauni, waziri wa mambo ya ndani, ujumbe wangu kwako leo ni mfupi tu. Huwenda usikuchukue hata dakika 5 kuusoma kwasababu siku hizi hata simu zangu hushiki tena.
Huwenda umesahau Wacha nikukumbushe, wizara unayoongoza ndiyo wizara iliyo na mawaziri wengi zaidi katika historia kuliko wizara yeyote Nchini na mawaziri asilimia zaidi ya 90 wameongoza wizara hiyo kwa miaka chini ya mitatu yaani mwaka mmoja hadi miaka miwili .
Wengi wao walitenguliwa na baadhi yao walijuzulu kılinda hishma zao na kumlinda Boss wao (Mh. Raisi).
Hii inadhihirisha ni namna gani unaongoza wizara yenye moto mkali ndani na nje.
Moja ya watangulizi wako ni Ali Hassan Mwinyi, Alijiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani kulinda hishma wake na hishma ya Rais wake, lakini kutokana na uungwana ule watu wakamfaa kumpa nafasi kubwa zaidi ya uraisi wa Zanzibar na baadae uraisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hautakuwa waajabu kupisha na kuwaachia wengine ili kulinda hishma yako bwana mkubwa. Wala hautakuwa wa kwanza kufanya hivyo.
Jina la Rais wetu limechafuka kila sehemu, ni wewe pekee utaweza kulisafisha kwa kuachia nafasi yako kutokana na matukio yanayoendelea Nchi nzima ya mauwaji na utekaji. Huwenda usiwe muhusika wa moja kwa moja na matukio haya, lakini matukio yanayoendelea yanaigusa wizara unayoiongoza moja kwa moja.
Muungwana akivuliwa nguo huchutama, hakuna mwenye shaka juu ya uungwana wako Bwana mkubwa, hebu chutama sasa utamalaki uungwana wako.
Nakukumbusha tu waislamu wana neno lao husema
“Man satara musliman satarallahu Yaumul Qiyama “
Soma Pia:
Wasalaam.

- Ushauri: Waziri wa Mambo ya Ndani jiuzulu, DCI aondolewe na Rais aunde tume inayojitegemea ifanye uchunguzi wa kina
- Waziri Hamad Yussuf Masauni, jiuzulu kumpunguzia Mzigo rais Samia. Anakuonea aibu
Wasalaam.