MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Mtihani wa darasa la nane umehitimishwa, kawaida tulizoea habari za visa vya udanganyifu miaka yote kila tukifikia mwisho. Lakini waziri na timu yake wamekomaa mwaka huu, waliibuka na mikakati mipya na kwa kweli imefua dafu.
Kila fununu ya tatizo lolote imekuwa ikishughulkiwa kwa nguvu nyingi sana. Watu wachache wamekamatwa kwa kujaribu kuchovya, wao huishi kwa mazoea.
Ama kwa kweli juhudi kama hizi zikitiliwa mkazo na maanani, tutakua na kizazi cha Wakenya wapya waadilifu, na wenye bidii kwenye masuala ya elimu. Maana tukiwanyoosha watoto wetu wakiwa wadogo, lazima hatimaye wataishia kuwa watu wanaostahili kwenye jamii. Taarifa za wazazi kuwanunulia watoto wao mitihani zilikua zinatamausha, maana ndio hapo mbegu ya ufisadi ilikua inafukiwa na kuota.
Kumdhihirishia mtoto kwamba kwa kuhonga anaweza akawa mshindi hata kwenye elimu ni jambo hatari sana kwa jamii. Bora aje na alama mbaya umsaidie kujiboresha lakini sio kumnunulia alama kwenye mtihani eti ndio ahitimu kuingia chuo kikuu. Hao ndio wanaishia kuwa wakurugezi vila.za wasiojua mwanzo au mwisho wa wanakoenda na wanakotoka.
Heko waziri kwa kazi nzuri, kweli tunaweza kushinda vita dhidi ya ufisadi tukimaanisha na bila kuwan na unafiki.