Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Aidha, kupitia mradi huu Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika na ya tano Duniani kwa kuwa na Mtandao mrefu zaidi wa reli ya SGR," amesema Mbarawa.
Amedai kuwa hatua hiyo itasaidia kuepusha uharibifu wa barabara, kuongeza mapato, kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kutoa huduma ya usafiri wa uhakika.
"Kuanza kwa huduma za usafiri katika reli ya kiwango cha kimataifa kutachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la pato la taifa pamoja na maendeleo ya shughuli nyingi za kiuchumi, kijamii na kiutawala kwa kutoa usafiri wa uhakika na wa haraka. Sekta ambazo zinatarajiwa kuguswa moja kwa moja na usafiri wa reli ya SGR ni pamoja na Biashara, Utalii, Viwanda, Kilimo, Uvuvi na Ufugaji," amesema Mbarawa.
Aidha ameeleza kuwa mpaka sasa Serikali imeshatumia kiasi cha Dola za Marekani bilioni 3.138 kwa ujenzi wa miundombinu ya SGR kwa vipande viwili vya Dar es Salaam - Morogoro-Makutopora Dodoma jumla ya kilomita 722, ambapo amesema kwamba kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro zimetumika Dola za Marekani Dola Bilioni 1.215 na kipande cha Morogoro hadi Makutopora Dodoma zimetumika Dola za Marekani Bilioni 1.923.
Ameyasema hayo Julai 30, 20 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelekea uzinduzi rasmi wa ruti ya Treini Dar es Salaam - Dodoma, ambao utafanyika August 1, 2024 Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.