LGE2024 Waziri Mchengerwa atangaza rasmi kukoma kwa madaraka ya viongozi wa vijiji na mitaa Tanzania

LGE2024 Waziri Mchengerwa atangaza rasmi kukoma kwa madaraka ya viongozi wa vijiji na mitaa Tanzania

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ameelekeza madaraka ya wenyeviti wa vijiji, wajumbe wa Halmashauri za Vijiji na Wenyeviti wa Vitongoji katika mamlaka za Wilaya, Miji na Mamlaka za miji midogo kukoma Oktoba 19, 2024 na nafasi zao kujazwa na viongozi watakaopatikana katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024

Mchengerwa ametoa maelekezo hayo Jijini Mwanza wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.

Pia ametoa mwongozo kuwa majukumu yote ya utendaji katika kijiji au mtaa yataendelea kutekelezwa kwa mujibu wa sheria na maafisa watendaji wa vijiji au mitaa kwa kushirikiana na maafisa watendaji wa kata husika.

Soma pia: Waziri Mchengerwa atangaza tarehe ya kuchukua na kurudisha Fomu za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, siku zaongezwa

Hata hivyo ametoa angalizo kuwa watendaji wa vijiji au mtaa hawataruhusiwa kutekeleza jukumu lolote la kisheria ambalo linapaswa kuamuliwa na Halmashauri ya Kijiji au Kamati ya Mtaa na endapo kutakuwa na jambo haliwezi kusubiri hadi Serikali ya Kijiji au Kamati ya Mtaa kuundwa, basi Afisa Mtendaji wa kijiji au mtaa husika ataliwasilisha kwa Afisa Mtendaji wa Kata ambaye atalazimika kuliwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika ili kupata idhini ya kulitekeleza.

Aidha, Waziri Mchengerwa ametoa rai kwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji na wenyeviti wa mitaa kuhakikisha ofisi na nyaraka muhimu zinakabidhiwa kwa watendaji wa vijiji na watendaji wa mitaa ifikapo Oktoba 19, 2024.


 
Back
Top Bottom