Waziri Mchengerwa: Hatutasita Kuchukua Hatua kwa Kiongozi Anayewanyanyasa Wananchi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAZIRI MCHENGERWA: HATUTASITA KUCHUKUA HATUA KWA KIONGOZI ANAYEWANYANYASA WANANCHI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI haitasita kuchukua hatua kwa kiongozi yeyote anayewanyanyasa wananchi kupitia ukusanyaji wa ushuru wa mazao kwani Serikali imeshakwisha kutoa Miongozo kuhusu ukusanyaji wa ushuru wa mazao.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati akichangia hoja yake bungeni jijini Dodoma katika Bunge la Bajeti ya mwaka 2024/2025 linaloendelea.

“yapo maeneo ambapo tunaona kuna hitulafu katika ukusanyaji wa ushuru wa mazao, tutafika huko katika Halmashauri zenye changamoto hizo, maelekezo yangu watanzania wasiyanyasike kwenye maeneo yao na TAMISEMI hatutasita kuchukua hatua kwa kiongozi yeyote anawanyanyasa Watanzania katika maeneo yetu kwani serikali ilikwisha kutoa muongozo”

Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema ifikapo tarehe 30 mwezi juni maandalizi juu ya utolewaji wa Mikopo ya asilimia 10 yatokanayo na mapato ya ndani ya Halmashauri yatakuwa yamekamilika na wataalamu kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI watafika katika Halmashauri zote nchini ili kutoa elimu ya utaratibu ulioboreshwa katika utolewaji wa Mikopo hiyo ili wanufaika wa mikopo hiyo wawezekunufaika.

Amesema Serikali imetenga zaidi ya Bil. 400 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika kila jimbo la uchaguzi kote nchini na kwaajili ya kujenga na kukarabati Hospitali za Halmashauri.

Pia, Mhe. Mchengerwa ameunga mkono hoja ya Bajeti iliyotolewa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais, Mipango na uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo aliyoitoa leo Bungeni Jijini Dodoma katika Bunge la Bajeti linaloendelea.
 
Mkumbushe viongozi wanaowanyanyasa wananchi wako pale bungeni ndani na Kila siku wanatunga sheria ngumu za kuumiza
 
Mh, anza na CHURA KIZIWI.
NI MNYANYASAJI HAKUNA WA KULINGANA NAYE.
KAUZA BANDARI,NGORONGORO,LOLIONDO nadhani akimalizana na MLIMA KILIMANJARO ZIWA VICTORIA na mbuga ya SERENGETI vitafuata.

Au vyote ameshauza wakuu?
 
Back
Top Bottom