LGE2024 Waziri Mchengerwa Kwa Wagombea: Acheni kufanya Propaganda zisizo na ukweli, zitakazoleta taharuki

LGE2024 Waziri Mchengerwa Kwa Wagombea: Acheni kufanya Propaganda zisizo na ukweli, zitakazoleta taharuki

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Waziri Mohamed Mchengerwa hivi karibuni amedokeza kuwa malalamiko yanayoendelea hivi sasa kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa kwa wingi wake ni propaganda zisizo na msingi.

Soma pia: Waziri Mchengerwa: Hakuna Uthibitisho wa madai ya Uandikishaji Wanafunzi Kupiga Kura

Wakati anazungumza na vyombo vya habari kuhusu mchakato wa kuchukua, kurejesha, uteuzi pamoja na rufaa za wagombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, Mchengerwa alisema kuwa:

"Acheni kufanya 'Propaganda' zisizo na ukweli na zinaweza kuleta taharuki inayoweza kudababisa uvunjifu wa amani, ni vyema kuendeleza kueleza Umma wa Watanzania ukweli na uhalisia wa vyama vya siasa katika uchaguzi huu wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji"

Source: Michuzi Blog
 
Huyu mzee kwa vile yupo chini ya mama mkwe anajiona yupo juu ya sheria anaweza kufanya ujinga wowote na hatuwezi kumfanya chochote huyu hewa
 
Kwa sasa hivi hapa Tanzania Mohamed Mchengerwa ndiye adui mkubwa wa demokrasia na lolote litakalotokea kutokana na ushenzi aliofanya kwenye mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa lawama zote atabeba yeye na uzao wake wote. Ni jitu la hovyo,lenye roho mbaya kumzidi ibilisi. Alaaniwe Mchengerwa na uzao wake wote,lolote mbaya limpate .
 
Akifuatiwa na mama mkwe wake
 
Back
Top Bottom