Waziri Mchengerwa: Natamani kuona kila mtumishi anasikilizwa kero zake

Waziri Mchengerwa: Natamani kuona kila mtumishi anasikilizwa kero zake

maiyanga1

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
1,340
Reaction score
1,832
Hayo ni maneno aliyoyasema Mchengerwa waziri wa Mali asili na Utalii jana tarehe 20/03/2023 kwenye kikao cha 30 cha baraza la wafanyakazi. Kwako Waziri, naamini ulisema hivyo kwa sababu unajua kwamba watumishi hawasikilizwi shida na kero zao.

Kuanzia hapo Mpingo house kuna maafisa utumishi ni miungu watu. Hawana muda wa kusikiliza watumishi, wamejawa na upendeleo, wanapandisha watumishi vyeo kwa kujuana au kwa pesa. Kwenye kanda, vituo na ofisi nyingi za TFS, kuna majungu, makundi, na uvunjifu mkubwa wa taratibu za utumishi.

Field Officers ambao ndio wanaofanya kazi ya kutekeleza sera mbalimbali hawasikilizwi. Mameneja, wakuu wa vituo na maofisa kazi yao kubwa ni kusafiri na kuhudhuria warsha, semina na mafunzo ambayo kwa asilimia kubwa huwa kwa ajili ya watendaji (field officers).

Mfano mafunzo ni ya siku tano yanaitaji field officer, atakwenda meneja au mkuu wa kituo, akirudi anamuita field officer kwa masaa machache na kumuelekeza alichofundishwa yeye kwa siku tano.

Waziri usiishie kusema, tengeneza mfumo utakaoondoa madudu yote hayo, ili kuboresha utendaji kazi.
 
Back
Top Bottom