DOKEZO Waziri Mchengerwa, nenda Nasibugani Sekondari Mkuranga, shule haina umeme, maji, madawati, walimu, vitanda wala barabara nzuri

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Retina

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2015
Posts
1,039
Reaction score
1,163
Shule hii kidato Cha I-VI, shule imepelekewa wanafunzi 400+ wa kidato cha tano huku hakuna miundombinu inayotosheleza kupokea idadi hiyo ya wanafunzi.

Shule ni kama imetelekezwa hakuna anayejali, watoto wetu wanalala chini, umeme hakuna shule ipo gizani wakati ipo porini, shule haina walimu wa kutosha kuwahudumia idadi kubwa ya wanafunzi, shule haina miundo mbinu ya maji, wanafunzi wanachota maji porini, nimemtembelea mdogo wangu hali niliyoikuta ni zaidi ya kile nilichokieleza hapo juu.

Nakuomba waziri Mchengerwa uwaokoe watoto wetu wanateseka, ikibidi ufike shuleni kabisa ujionee, usiwasikilize. Viongozi wa Mkuranga ikiwemo Afisa Elimu, Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya watakudanganya.

Fika shuleni uongee na wanafunzi au walimu.
 
Shule hii kidato Cha I-VI,shule imepelekewa wanafunzi 400+ wa kidato Cha tano huku hakuna miundo mbinu inayotosheleza kupokea idadi hiyo ya wanafunzi...
Haaaa 😳😳😳!! Hakyanani lawama zote ziende kwa MACHADEMA!
 
Waziri mteule akafanye nini huko?
Ingekua mkutano wa vijembe vya CCM dhidi ya upinzani angekwenda Jana.
Mwacheni waziri wetu ale Bata.
 
Shule hii kidato Cha I-VI, shule imepelekewa wanafunzi 400+ wa kidato cha tano huku hakuna miundombinu inayotosheleza kupokea idadi hiyo ya wanafunzi.

Shule ni kama imetelekezwa hakuna anayejali, watoto wetu wanalala chini, umeme hakuna shule ipo gizani wakati ipo porini, shule haina walimu wa kutosha kuwahudumia idadi kubwa ya wanafunzi, shule haina miundo mbinu ya maji, wanafunzi wanachota maji porini, nimemtembelea mdogo wangu hali niliyoikuta ni zaidi ya kile nilichokieleza hapo juu.

Nakuomba waziri Mchengerwa uwaokoe watoto wetu wanateseka, ikibidi ufike shuleni kabisa ujionee, usiwasikilize. Viongozi wa Mkuranga ikiwemo Afisa Elimu, Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya watakudanganya.

Fika shuleni uongee na wanafunzi au walimu.
Mchengerwa ana kifua kipana kumkumbatia binti Saa 100. Hilo la Mkuranga Seko lisubiri mkwe amalizane na mjomba DP world faraghani
 
Wakat huku Moshi shule Ina wanafunzi 164
Walimu 26
 
Hiyo habari ni ya kuichezea Serikali
 
Wakat huku Moshi shule Ina wanafunzi 164
Walimu 26
Moshi sio Tanzania labda!! Shule nzima iwe na wanafunzi 164?? Wakati kibongo bongo huu ni mkondo mmoja, sio darasa zima??

Sio kweli!!

Weka jina la (iwe ya serikali) nipigwe life BAN
 
Shule hii kidato Cha I-VI, shule imepelekewa wanafunzi 400+ wa kidato cha tano huku hakuna miundombinu inayotosheleza kupokea idadi hiyo ya wanafunzi.

Shule ni kama imetelekezwa hakuna anayejali, watoto wetu wanalala chini, umeme hakuna shule ipo gizani wakati ipo porini, shule haina walimu wa kutosha kuwahudumia idadi kubwa ya wanafunzi, shule haina miundo mbinu ya maji, wanafunzi wanachota maji porini, nimemtembelea mdogo wangu hali niliyoikuta ni zaidi ya kile nilichokieleza hapo juu.

Nakuomba waziri Mchengerwa uwaokoe watoto wetu wanateseka, ikibidi ufike shuleni kabisa ujionee, usiwasikilize. Viongozi wa Mkuranga ikiwemo Afisa Elimu, Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya watakudanganya.

Fika shuleni uongee na wanafunzi au walimu.

Leo tarehe 01/07/2023, nilienda kutembelea shule ya sekondari yenye kidato cha I-vi Nasibugani high school , shule hii ipo tarafa ya Kisiju, kata ya Msonga halmashauri ya wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, ipo km 48 toka halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, kijana wangu amechaguliwa kusoma tahasusi ya CBG. Ilibidi nifunge safari kimya kimya mpaka Nasibugani huko Mkuranga.

Hii shule unaweza kusema imetelekezwa, haina miundo mbinu ya kukidhi wanafunzi kusoma, licha kidato cha tano na sita tangu 2015.

1. Kuifikia hiyo shule haina barabara rasmi. Kutoka Mkuranga unapanda basi hadi kituo kinaitwa mavunja, ukitoka mavunja unapanda pikipiki mpaka eneo la wazi kipindi cha masika wanafunzi wanavushwa na mtumbwi hii ni hatari sana.

2. Haina miundombinu ya maji, kuna tanki moja na kisima kimoja ambacho hakikidhi mahitaji ya wanafunzi

3. Haina umeme wa gridi ya taifa licha ya umeme huo ukiishia kijijin, mita 800 toka shule.Tangu 2015-2023 shule inatumia miundo mbinu ya umeme wa jua ambayo ni mibovu baadhi ya mabweni hayana solar wakati shule imezungukwa na mapori.

4. Shule haina hospital inayokidhi mahitaji ya wanafunzi kiafya. Kituo cha afya kipo km.10+ toka shule,barabara ni ile yenye swamp ambayo kwenye masika haipitiki, kwa dharura haifai.

TAMISEMI njooni muione hii shule.

Wewe sio mzazi!! Sema wewe ni nani??

Bado hujasema, mpaka useme!!!

Utasema tu!!
 
Shule hii kidato Cha I-VI, shule imepelekewa wanafunzi 400+ wa kidato cha tano huku hakuna miundombinu inayotosheleza kupokea idadi hiyo ya wanafunzi.

Shule ni kama imetelekezwa hakuna anayejali, watoto wetu wanalala chini, umeme hakuna shule ipo gizani wakati ipo porini, shule haina walimu wa kutosha kuwahudumia idadi kubwa ya wanafunzi, shule haina miundo mbinu ya maji, wanafunzi wanachota maji porini, nimemtembelea mdogo wangu hali niliyoikuta ni zaidi ya kile nilichokieleza hapo juu.

Nakuomba waziri Mchengerwa uwaokoe watoto wetu wanateseka, ikibidi ufike shuleni kabisa ujionee, usiwasikilize. Viongozi wa Mkuranga ikiwemo Afisa Elimu, Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya watakudanganya.

Fika shuleni uongee na wanafunzi au walimu.
Shule ni kama imetelekezwa hakuna anayejali, watoto wetu wanalala chini, umeme hakuna shule ipo gizani wakati ipo porini, shule haina walimu wa kutosha kuwahudumia idadi kubwa ya wanafunzi, shule haina miundo mbinu ya maji, wanafunzi wanachota maji porini, nimemtembelea mdogo wangu hali niliyoikuta ni zaidi ya kile nilichokieleza hapo juu.[emoji3064][emoji3064][emoji3064]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KONDOA huko ndani ndani, Shule ya Msingi ina walimu 6... ina madarasa yote I - VII... yaani walimu wote wakiingia madarasani kuna darasa linabaki bila Mwl
 
Back
Top Bottom