Mmezidi kulalamika. Halafu kwenye uchaguzi mnapewa vijilaki mnasahau shida zenu na kusheherekea raha za muda mfupi. Huyo mkurugenzi muendeeni Gamboshi hapo mmalizane nae.Mheshimiwa Waziri,
Sisi, walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, tunakuandikia kwa huzuni na wasiwasi mkubwa kuhusu vitendo vya ukaidi na unyanyasaji tunavyopata kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Ndugu Marco Kachoma. Tangu mwezi wa Agosti 2024, tulipomuandikia barua rasmi ya kujitoa kutoka Chama cha Walimu (CWT) na kujiunga na Chama cha Kutetea Maslahi ya Walimu (Chakuhawata), tumekuwa tukikabiliwa na vikwazo na manyanyaso yasiyo na msingi.
Licha ya haki yetu ya kikatiba ya kujiunga na chama chochote tunachokiona kinafaa kutetea maslahi yetu, Ndugu Kachoma amekuwa akituzuia na kutishia usalama wetu wa ajira. Hadi sasa, walimu wapatao 150 walioamua kuhamia Chakuhawata wameendelea kupokea vitisho kutoka kwa Mkurugenzi huyu. Tumekuwa tukinyimwa fursa za kushiriki na kusimamia matukio muhimu ya kitaifa kama vile mitihani, jambo ambalo limeathiri sana morali na utendaji wetu wa kazi.
Mbaya zaidi, Kaimu Katibu wa Chakuhawata ameendelea kutishwa na kuhofia kufukuzwa kazi endapo ataendelea kusimamia na kudai haki za walimu. Kutokana na hali hii, tuliamua kumuandikia Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, tukimuelezea juu ya ukaidi wa Ndugu Marco Kachoma. Kwa uchungu, tunaripoti kwamba hadi sasa, licha ya barua kutoka kwa Katibu Mkuu iliyomuelekeza Ndugu Kachoma kuzingatia kanuni na sheria za ajira, hakutekeleza agizo hilo. Kuanzia mwezi wa Novemba 2024 hadi leo hii tarehe 22 Januari 2025, hatujaondolewa rasmi kutoka CWT na kuungwa rasmi na Chakuhawata kama ilivyotarajiwa.
Tumechukua hatua zaidi kwa kuwasilisha malalamiko yetu kwa Mkuu wa Wilaya ya Busega pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Busega, lakini bado hali haijabadilika. Vitendo vya Ndugu Kachoma vimetusababishia uchungu mwingi na kutuondolea kabisa morali ya kufanya kazi.
Kwa heshima tunakuomba, Mheshimiwa Waziri, uchukue hatua stahiki ili kuhakikisha kuwa haki zetu kama walimu zinaheshimiwa na tunapata mazingira bora ya kazi. Tunakuomba uzingatie malalamiko haya kwa uzito unaostahili na kuchukua hatua dhidi ya Ndugu Marco Kachoma kwa kuzingatia sheria na kanuni za ajira.
Asante kwa wakati wako na tunategemea msaada wako katika suala hili.
Wako kwa dhati,
[WALIMU 150 TUNAOIKANA CWT]
[WANACHAMA]
Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega
MY TAKE: KAMA HUYU MKURUGENZI HAMHESHIMU KATIBU MKUU KIONGOZI IKULU JE ATATUHESHIMU SISI WALIMU NA WAFANYAKAZI WAKE TULIO CHINI YAKE? TAFAKARI, CHUKUA HATUA
View attachment 3210478
Tutamalizana kisheria tuMmezidi kulalamika. Halafu kwenye uchaguzi mnapewa vijilaki mnasahau shida zenu na kusheherekea raha za muda mfupi. Huyo mkurugenzi muendeeni Gamboshi hapo mmalizane nae.
Sio rahisi kihivoBye bye bwana rafael karibu mtaani soon
Umesoma kilichoandikwa na kiambatanisho Chake,au wewe ni miongoni mwa watoa ushauri bila kumsikiliza client wako?Kazi hawezi wafukuza, TSC ndiyo anafukuza.kusimamia mitihani sio lazima,uchaguzi mkuu atawaita tu.la msingi fanyeni kazi kufuata Sheria.shughuli za chama fanyeni weekend.
Asante sana,sielewi kabisa hawa watendaji waserikali kuwa chanzo Cha migogoro mahali pa kazi
Hadi katibu mkuu kiongozi ikulu amemwambia alitekekeleze,lakini toka mwezi wa 11 Hadi Muda huu Bado,huyu jamaa Kachoma anajeuri sana sijawahi ona,serikali iingilie katiJambo lipo kisheria kwanini anapata kigugumizi kulitekeleza?
Why!? Unachuki na Mwalimu?MIMI NIKISIKIA WALIMU ni humu tu
View attachment 3215327
Mtu yoyote ambaye anashindwa kutumia akili zake kama walimu nawachukia. Hawa walimu WANAJUA TU KUIBA KURA alafu wanakuja kututilia huruma. Wacha yanyooshwe tu hayana Maana yananunulika kwa ten tenWhy!? Unachuki na Mwalimu?
Inauma sana,huyu mkurugenzi Kachoma anadai amewahi kuwa mwalimu lakini tabia na mienendo yake haifai, ni mtu mwenye kiburi na ubabe,nadhani serikali itatisaidia juu ya huyu bwanaTatizo la nchi hii ni mfumo, huyo anaweza akawa kipenzi(mtu wa karibu) wa mheshimiwa hivyo anajua hawa wengine hawana jeuri na ikizidi sana ni anahamishwa tu kitengo.
"Ukiona swala anatembea kwa maringo mbugani ujue simba ndio bwana wake."
Anadharau kwa mamlaka yake ya Uteuzi na wale anaowatumikia. Utaratibu wa kutumbua majipu urudiweMheshimiwa Waziri,
Sisi, walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, tunakuandikia kwa huzuni na wasiwasi mkubwa kuhusu vitendo vya ukaidi na unyanyasaji tunavyopata kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Ndugu Marco Kachoma. Tangu mwezi wa Agosti 2024, tulipomuandikia barua rasmi ya kujitoa kutoka Chama cha Walimu (CWT) na kujiunga na Chama cha Kutetea Maslahi ya Walimu (Chakuhawata), tumekuwa tukikabiliwa na vikwazo na manyanyaso yasiyo na msingi.
Licha ya haki yetu ya kikatiba ya kujiunga na chama chochote tunachokiona kinafaa kutetea maslahi yetu, Ndugu Kachoma amekuwa akituzuia na kutishia usalama wetu wa ajira. Hadi sasa, walimu wapatao 150 walioamua kuhamia Chakuhawata wameendelea kupokea vitisho kutoka kwa Mkurugenzi huyu. Tumekuwa tukinyimwa fursa za kushiriki na kusimamia matukio muhimu ya kitaifa kama vile mitihani, jambo ambalo limeathiri sana morali na utendaji wetu wa kazi.
Mbaya zaidi, Kaimu Katibu wa Chakuhawata ameendelea kutishwa na kuhofia kufukuzwa kazi endapo ataendelea kusimamia na kudai haki za walimu. Kutokana na hali hii, tuliamua kumuandikia Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, tukimuelezea juu ya ukaidi wa Ndugu Marco Kachoma. Kwa uchungu, tunaripoti kwamba hadi sasa, licha ya barua kutoka kwa Katibu Mkuu iliyomuelekeza Ndugu Kachoma kuzingatia kanuni na sheria za ajira, hakutekeleza agizo hilo. Kuanzia mwezi wa Novemba 2024 hadi leo hii tarehe 22 Januari 2025, hatujaondolewa rasmi kutoka CWT na kuungwa rasmi na Chakuhawata kama ilivyotarajiwa.
Tumechukua hatua zaidi kwa kuwasilisha malalamiko yetu kwa Mkuu wa Wilaya ya Busega pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Busega, lakini bado hali haijabadilika. Vitendo vya Ndugu Kachoma vimetusababishia uchungu mwingi na kutuondolea kabisa morali ya kufanya kazi.
Kwa heshima tunakuomba, Mheshimiwa Waziri, uchukue hatua stahiki ili kuhakikisha kuwa haki zetu kama walimu zinaheshimiwa na tunapata mazingira bora ya kazi. Tunakuomba uzingatie malalamiko haya kwa uzito unaostahili na kuchukua hatua dhidi ya Ndugu Marco Kachoma kwa kuzingatia sheria na kanuni za ajira.
Asante kwa wakati wako na tunategemea msaada wako katika suala hili.
Wako kwa dhati,
[WALIMU 150 TUNAOIKANA CWT]
[WANACHAMA]
Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega
MY TAKE: KAMA HUYU MKURUGENZI HAMHESHIMU KATIBU MKUU KIONGOZI IKULU JE ATATUHESHIMU SISI WALIMU NA WAFANYAKAZI WAKE TULIO CHINI YAKE? TAFAKARI, CHUKUA HATUA
View attachment 3210478
Ni kweli,toka apewe maelekezo Leo ni miezi takribani mitatu,Sasa unabaki kujiuliza je huyu mkurugenzi ni mkubwa kuliko mamlaka yake ya uteuzi au ni kiburi Cha madaraka?Anadharau kwa mamlaka yake ya Uteuzi na wale anaowatumikia. Utaratibu wa kutumbua majipu urudiwe