Waziri Membe: Katiba mpya itambue uwepo wa Diaspora na Uraia wa nchi mbili.

Waziri Membe: Katiba mpya itambue uwepo wa Diaspora na Uraia wa nchi mbili.

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,503
“Uwepo wa Diaspora ni lazima utambulike Kikatiba,” amesema Waziri Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Waziri Membe aliyasema hayo alipokutana na Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo katika Ofisi za Tume hiyo zilizopo mjini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao walijadili suala la uraia wa nchi mbili (dual citizenship) ambalo linapiganiwa kwa kiasi kikubwa na Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora).

“Tumekuja kuwasilisha masuala muhimu mawili: moja, uwepo wa uraia wa nchi mbili katika Rasimu ya Katiba na pili, Katiba mpya iruhusu raia yoyote wa Tanzania aweze kuwa na uraia wa nchi nyingine pasipo kuukana uraia wa Tanzania,” alieleza Waziri Membe.

Alisema kuwa Wizara yake inatambua suala la uraia wa nchi mbili kuwa ni la msingi, ambalo halikugusiwa katika Rasimu ya Katiba iliyopo.

“Chimbuko la uraia wa nchi mbili lilitokana na wingi wa Watanzania walioko nje ya nchi ambao wanatafuta fursa ya kuwekeza na kuinua maendeleo ya nchi yao,” alisema Waziri Membe.

Aliongeza pia, “Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005 inawatambua Watanzania hao na kutaka wapewe fursa ya kuwa na uraia wa nchi mbili katika kuinua maendeleo ya nchi.”

Watanzania hao wamekuwa wakikabiliana na matatizo kadhaa ambayo yanawanyima haki za msingi, kama vile afya, elimu na masuala ya ajira. “Kilio chao kimekuwa kero kubwa kwa vile wakati mwingine wanatibiwa kwa gharama kubwa sana ambazo hazilingani na kipato chao,” alisema Waziri Membe.

Aidha, changamoto hizo zimekuwa ni chanzo kikubwa cha kuwashawishi Watanzania hao kuchukua uraia wa nchi za kigeni ili kuwawezesha kupata huduma muhimu za kijamii kama vile elimu na afya.

“Hivi sasa sheria yetu haimruhusu Mtanzania kuchukua uraia wa nchi mbili pasipo kuukana uraia wa nchi yake,” alisema Membe, na kufafanua kuwa “Ilani ya CCM inamuhamasisha Mtanzania huyo achangie maendeleo ya nchi yake kupitia uraia wa nchi mbili.”

Waziri Membe alisema kuwa Watanzania wakiwa nje wanakosa fursa za kazi zenye kipato kikubwa wasipokuwa na uraia wa nchi hiyo, jambo linalopelekea maisha magumu na kushindwa kujikimu na kuchangia kipato chochote kwa ndugu zao walioko nchini.

“Badala yake, unakuta Watanzania wananaswa na tamaa ya ‘kujilipua’ kwa kubadili uraia wa nchi nyingine zinazokubali uraia wa nchi mbili na kuachana na uraia wa Tanzania,” alieleza Waziri Membe.

Kwa upande wake, Mhe. Warioba alisema kuwa maoni hayo ya uraia wa nchi mbili yamekuwa yakijitokeza katika ukusanyaji wa maoni sehemu mbalimbali. Na kuongeza kuwa, hofu kubwa ya wananchi ni usalama wa nchi yao endapo uraia wa nchi mbili utaruhusiwa.

Mhe. Waziri Membe alikuwa ameambatana na Balozi Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Bertha Semu-Somi, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora na Bw. James Lugaganya, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kwa upande wa Mhe. Warioba, alikuwepo Jaji Mkuu Mstaafu Agostino Ramadhani, Makamu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Salim Ahmed Salim, Mjumbe wa Tume, pamoja na Katibu na Naibu Katibu wa Tume ya Mabadiliko.
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    41.4 KB · Views: 92
  • image.jpg
    image.jpg
    27.6 KB · Views: 92
  • image.jpg
    image.jpg
    29.5 KB · Views: 97
This is good news kwa watembezi watembezi kama sisi na vile vile ni good news kwa taifa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kuna watu wanapenda direct kutoa mchango wao kisiasa lakini string attached na sheria za nchi zinawafanya washindwe kufanya hivyo.

Kuna watu wanataka kuwekeza kiuchumi nchini lakini sheria na urasimu unawafanya wasite au washindwe kufanya hivyo.

Kuna watu wanapenda na wanataka kutoa michango yao ya hali na mali lakini mazingira ya kijamii yanawazuia kufanya hivyo kama 'wageni'.

This is a win win situation kwa Tanzania na watembezi wa kitanzania.
 
Kwa nini Membe asipeleke mswada huo bungeni ujadiliwe na kupigitishwa sheria mbadala kuruhusu hii kitu badala ya danadana inayoendelea kupitishwa kwa kutumia katiba.

Hoja ya kamati ya katiba ina ukweli fulani, suala la uhamiaji huwa linabadilikabadilika kutokana na mazingira fulanifulani, bora ikapitishwa tu kama sheria ya uhamiaji badala ya kuendelea na hii danadana ya kuipenyeza kwenye katiba wakati hoja ya hao wataalamu ina mshiko.
 
Mkuu Candid Scope Kumbuka katiba ni sheria mama na kwa sasa inaelekea tutakuwa na serikali mbili au tatu zinazotokana na nchi mbili tofauti zitakazoungana. Kwa mantiki hiyo, kuweka swala la uraia wa nchi mbili kwenye katiba ya Muungano ni muhimu kuliko kutunga sheria ambazo baadaye zinaweza kuwa incompatible na sheria za nchi moja au nyingine.

Hili swala kutambuliwa na katiba ya Jamhuri wa Muungano ni muhimu sana ili kuepuka matatizo yatakayojitokeza mbele ya safari kama chama au 'Rais mwingine'(independent) ambaye sera zake ziko kinyume na hili swala ataingia madarakani kwa sababu process ya kubadilisha katiba ya Jamhuri siyo rahisi kama ilivyo process ya kutunga na kubadilisha sheria za nchi mojawapo zilizoko kwenye muungano.

Baada ya kutambuliwa na Katiba ya Muungano, itakuwa rahisi kutungiwa sheria kuhusu namna ambavyo sheria ya uraia wa nchi mbili unakuwa ndani ya serikali tatu na katika nchi mbili kulingana na nchi.
 
Ukiangalia nchi nyingi suala la uhamiaji lina sheria ambazo hubadilikabadilika mara kwa mara na hivyo halijaingizwa rasmi kwenye katiba ya nchi hizo, ila lipo kwenye sheria za uhamiaji za nchi husika.

Kwa kesi ya nchi yetu suala la uhamiaji ni tata kwa katiba mpya kutokana na kwamba inavyoelekea Zanzibar wana katiba yao, hivyo basi Wataanganyika tunahitaji katiba yetu humo ndimo kungewekwa masuala haya kwa uwazi na kwamba raia wa visiwani wana mipaka gani kama mipaka tuliyowekewa wabara kule visiwani.

Tatizo ninaloliona Membe anashindwa kupenyeza pale bungeni mswada huo na kuutetea kama anavyofanya sasa. Nafikiri kwanza sheria hiyo ingetungwa kwanza ianze kufanya kazi yake wakati suala la kutambuliwa kikatiba itakapohitajika linaweza kuingizwa hata baadaye kama amendment. Membe apeleke mswada bungeni kama sheria ya uahamiaji ianze kufanya kazi ndilo tunalotaka lakini hii danadana ya kusingizia katiba mpya ni kupoteza wakati wakati wanaohitaji hiyo wanazidi kufa njaa.
 
Kutambua Dispora sawa hatuna tatizo,
Lakini hilo la kujifanya Sigara Kali au Waliberal yani tupo huku na huku aka Nchi Mbili, kwangu Halikubaliki kamwe!
 
Kutambua Dispora sawa hatuna tatizo,
Lakini hilo la kujifanya Sigara Kali au Waliberal yani tupo huku na huku aka Nchi Mbili, kwangu Halikubaliki kamwe!

Kwa hoja ipi, jaribu kuleta utetezi wako kujenga hoja ya kutushawishi maana vigezo alivyotoa Membe unajenga hoja gani ya kuvipinga?
 
Ukiangalia nchi nyingi suala la uhamiaji lina sheria ambazo hubadilikabadilika mara kwa mara na hivyo halijaingizwa rasmi kwenye katiba ya nchi hizo, ila lipo kwenye sheria za uhamiaji za nchi husika.

Kwa kesi ya nchi yetu suala la uhamiaji ni tata kwa katiba mpya kutokana na kwamba inavyoelekea Zanzibar wana katiba yao, hivyo basi Wataanganyika tunahitaji katiba yetu humo ndimo kungewekwa masuala haya kwa uwazi na kwamba raia wa visiwani wana mipaka gani kama mipaka tuliyowekewa wabara kule visiwani.

Tatizo ninaloliona Membe anashindwa kupenyeza pale bungeni mswada huo na kuutetea kama anavyofanya sasa. Nafikiri kwanza sheria hiyo ingetungwa kwanza ianze kufanya kazi yake wakati suala la kutambuliwa kikatiba itakapohitajika linaweza kuingizwa hata baadaye kama amendment. Membe apeleke mswada bungeni kama sheria ya uahamiaji ianze kufanya kazi ndilo tunalotaka lakini hii danadana ya kusingizia katiba mpya ni kupoteza wakati wakati wanaohitaji hiyo wanazidi kufa njaa.
Mkuu Candid Scope huoni kuwa kufanya mabadiliko kwa sasa ndani ya katiba hii ya 1977 ambayo 2015 itakuwa kaput ni kupoteza muda na pesa kwa malipo ya wabunge ambao watakuja tena kujadiri swala hilo hilo kwenye bunge la katiba.

Mimi ninafikiri ni vizuri tu kipengele kikawekwa kwenye katiba ijao ambayo itawafanya watembezi watembezi kujihusisha kikamilifu katika maswala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii baada ya katiba ya Muungano na 'Tanganyika' kama itakuja kuanza kutumiza huku sheria ya Zanzibar ikihitaji amendmend.
 
Last edited by a moderator:

Sina maana kwamba suala hilo lisijadiliwe na bunge ila kuna jambo moja inatakiwa tuwe kwenye mstari mmoja ndugu mleta mada.
Kwamba suala la uhamiaji kadiri ya waratibu wa Katiba mpya si suala la kuingizwa rasmi kwenye katiba kwa vile ni jambo linalobadilika mara kwa mara kutokana na mahitaji, mazingira na matukio. Katiba kwa kawaida ni kitu cha kudumu hakibadilikibaadiliki.

Hivyo basi suala hili haingetakiwa kulipotezea muda kama anavyofanya Waziri Membe, ila inatakiwa alipeleke moja kwa moja kwenye bunge kama mswada kama inavyotokea kwa sheria mbalimbali ambazo hazijaingizwa kwenye katiba. Hatua hii ingefanyika jambo hili lingeshapatiwa ufumbuzi mapema. Binafsi nakubaliana na hoja ya waratibu wa katiba mpya kwamba sheria za uhamiaji hubadilika mara kwa mara, hivyo liingizwe kwenye sheria za jumla za uhamiani. Huo ni mtazamo wangu baada ya kuwasoma hawa wataalamu waratibu wa Katiba mpya.

Jumanne wiki iliyopita tulijadili jambo hili tukiwa kwenye kijiwe pale Temeke na Diwani wa Kurasini Mr. Kimati, alisema tatizo ni watendaji wa serikali kujikanganya, hawako straight, vingievyo mambo mengi yasintekuwa kama yanavyoonekana kuwa magumu kupatiwa ufumbuzi.
 
Membe km waziri wa mambo ya nje amechukua hatua gani na jitihada gn kumaliza tofauti za kidlomasia kati ya tz na rwanda??
 
Kwanini apendekeze uraia wa nchi mbili badala ya tatu au zaidi?
 
Back
Top Bottom