Waziri Mhagama Aagiza Vituo vya Afya Visivyofuata Sheria Kushughulikiwa

Waziri Mhagama Aagiza Vituo vya Afya Visivyofuata Sheria Kushughulikiwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAZIRI MHAGAMA AAGIZA VITUO VYA AFYA VISIVYOFUATA SHERIA KUSHUGHULIKIWA

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama ameitaka Bodi ya 11 ya Ushauri ya Hospitali Binafsi kuhakikisha vituo vinavyoomba usajili vinakidhi vigezo vyote vya utoaji wa huduma bora za afya kabla yakupatiwa usajili pamoja na kufuatilia vituo vyote ambavyo vinatoa huduma bila usajili ili kupunguza malalamiko na changamoto kwa wananchi.

"Bodi hii pia, ina jukumu kubwa la kufanya ukaguzi wa vituo vya afya vilivyosajiliwa na kuhakikisha vinatoa huduma bora za afya kwa wananchi na kwa kuzingatia ngazi ambayo kituo hicho kimesajiliwa lakini vituo vinavyokiuka miongozo ya utoaji wa huduma iliyowekwa na Wizara mnatakiwa kuvichukulia hatua bila kuogopa lakini bila kuonea mtu.

"Sisi kama Serikali, tunao wataalamu. Tuna viongozi, wakaguzi na wasimamizi, wote kwa pamoja tufanye kazi kwa kusimamiana, na wote watakaotaka kuharibu mifumo yetu hao lazima tushughulike nao. Tumeshakubaliana kuwa Sekta Binafsi sio mshindani bali ni mshirika," amesema Waziri Mhagama

Waziri ametoa maelekezo hayo wakati akizindua Bodi hiyo mpya ya 11 ya Ushauri ya Hospitali Binafsi yenye wajumbe sita, inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Dkt. Grace Magembe ambae ni Mganga Mkuu wa Serikali.
 

Attachments

  • Screenshot 2025-03-06 at 13-07-48 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2025-03-06 at 13-07-48 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    601.1 KB · Views: 1
  • Screenshot 2025-03-06 at 13-07-38 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2025-03-06 at 13-07-38 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    547.6 KB · Views: 1
  • Screenshot 2025-03-06 at 13-07-28 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2025-03-06 at 13-07-28 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    679.7 KB · Views: 1
  • Screenshot 2025-03-06 at 13-07-16 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2025-03-06 at 13-07-16 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    658.7 KB · Views: 1
  • Screenshot 2025-03-06 at 13-07-03 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2025-03-06 at 13-07-03 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    703.2 KB · Views: 2
  • Screenshot 2025-03-06 at 13-06-44 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2025-03-06 at 13-06-44 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    615.9 KB · Views: 2
  • Screenshot 2025-03-06 at 13-05-53 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2025-03-06 at 13-05-53 Wizara Ya Afya (@wizara_afyatz) • Instagram photos and videos.png
    695.1 KB · Views: 1
Kutoka kuwa mwl wa Sec, had kuwa Waziri wa Afya.
Kweli Ndumba zinalipaa, msumbijii hoyeee! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom