JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkenda ametoa agizo hilo Julai 26, 2024 jijini Dodoma wakati akizungumza katika Kongamano la Utoaji Chakula na Lishe Shuleni, akisisitiza mzazi anayekataa kuchangia mchango uliowekwa kulingana na miongozo waliyojiwekea Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaweza kuchukua hatua dhidi ya mzazi wakati Mwanafunzi akiendelea na masomo.
"Lishe bora shuleni ni msingi muhimu katika maendeleo ya kiafya na kiakili na kwamba inachangia Mwanafunzi kujifunzaji kwa ufanisi. Mwanafunzi anapokosa chakula hukabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo njaa, utoro wa rejareja na hata kukatisha masomo kwa baadhi yao," alisema Mkenda.
Chanzo: Wizara ya Elimu
=========
Pia soma...
~ Wazazi wa wanafunzi Shule ya Sekondari BUJUNANGOMA, tumechoka na Michango, Rushwa, Utumikishwaji wa watoto wetu shuleni
~ Shule ya Msingi Tumaini ya Tabata Kimanga Wanafunzi wasiochangia Tsh. 800 wanatolewa Darasani
~ Malalamiko yaendelea kuhusu malipo ya 'Mchango wa Uendeshaji wa Shule Tsh 65,000' licha ya Serikali kufuta ada
~ Wanafunzi wa darasa la 7 shule ya Msingi Chanika wazuiliwa kuingia darasani kutokana na kutochangia 500 ya masomo