Malafyale
Platinum Member
- Aug 11, 2008
- 13,833
- 11,173
WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, amesema hajui kama Tanzania itaweza kuondokana na tatizo la rushwa na ufisadi, licha ya juhudi mbalimbali zinazochukuliwa na serikali kukabiliana na tatizo hilo.
Mkulo alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka unaoikutanisha serikali na wahisani, kutathimini mafanikio, na maeneo ambayo hakukuwa na mafanikio katika bajeti iliyopita.
Sijui kama Tanzania itaweza kuondokana na suala la rushwa na ufisadi, alisema Waziri Mkulo.
Kauli hiyo ya Mkulo ilitokana na swali la mwandishi wa habari aliyetaka kiongozi huyo afafanue zaidi kuhusu suala la rushwa alilolizungumza wakati wa hotuba yake ya ufunguzi, ambapo aliwahakikishia wahisani kuwa serikali inachukulia suala la rushwa kwa umakini sana.
Akifafanua suala hilo, Mkulo alisema kuna hisia kwamba serikali haijalivalia njuga suala la rushwa jambo ambalo si kweli.
Aliongeza kusema kuwa suala la rushwa ni gumu kukabiliana nalo kutokana na kuhusisha watu wawili, yaani mtoaji na mpokeaji.
Kupambana na rushwa ni jambo ambalo halichukui mwaka mmoja ukasema umepambana na rushwa, linachukua miaka. Kwa mfano mwaka 2004 tulikuwa na kesi 58 mahakamani na mwaka huu wa 2009 tuna kesi 1,578 za rushwa.
Hapo huwezi kusema hatujafanya juhudi suala la rushwa ni suala gumu na Sijui kama tutaweza kuondoka katika rushwa, lakini tunajitahidi, alisema Mkulo.
Mbali na hilo, akijibu swali kama pesa za safari na makongamano zinazotumiwa na viongozi ni za wafadhili, Mkulo alisema fedha hizo si za wafadhili, licha ya kwamba mikutano na makongamano yamekuwa mengi.
Kama alivyosema Waziri Mkuu, mikutano na makongamano hayo ni suala la kufikiria na kujaribu kutazama kama kweli yote yana maana, kwa hiyo ni suala la kufikiria, alisema.
Akizungumzia mkutano huo wa wiki nzima uliofunguliwa jana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mkulo alisema ni muhimu kwa kuwa serikali na wahisani walikubaliana kusaini misaada ya bajeti.
Alisema kila mwaka serikali na wahisani wanakutana na kukubaliana vigezo na nchi wahisani wanaahidi kiasi cha pesa kwa ajili ya kuchangia kwenye bajeti.
Mkulo alisema mkutano huo unatathimini yote yaliyofanikiwa katika kipindi cha mwaka uliopita na kwamba pale ambako serikali imeshindwa kufanikisha, inajieleza kwanini imeshindwa.
Waziri huyo wa fedha alisema kuwa wamekuwa na mazungumzo katika maeneo mengi na wahisani na wamekubaliana katika maeneo machache, ikiwamo katika eneo la uchumi.
Akielezea eneo ambalo kwa mwaka huu serikali imekwama katika kutekeleza maendeleo yake kama walivyokubaliana, Mkulo alilitaja eneo la kupunguza umaskini kupitia mkakati wa MKUKUTA.
Alisema kwenye kupunguza umaskini, kasi haikuwa kubwa kama ambavyo walitarajia hadi kufikia mwaka 2015 kwamba umaskini uwe umepungua kwa asilimia 50 ????????????.
Alizitaja sababu za kushindwa kupunguza umaskini kuwa ni pamoja na kilimo kuwa cha kusuasua, ubovu wa miundombinu, hususani barabara na mvua ambazo walitegemea zingenyesha, lakini hazikunyesha ???????.
Aidha, akizungumzia suala zima la bajeti, Mkulo alikiri kulikuwa na upungufu katika miezi ya Julai na Agosti, lakini ilipofika Septemba hali iliweza kurejea vizuri.
Alisema pia kulikuwa na pengo la sh bilioni 500 katika bajeti na walikubalina na Shirika la Fedha Duniani (IMF) waweze kukopa asilimia 1.5 katika pato la ndani.
Mkutano huo wa wiki moja, unawakutanisha wahisani, wadau mbalimbali katika masuala ya bajeti pamoja na serikali.