Waziri Mkuu ashtuka kusikia Madereva wa Serikali wanalogana wapate kazi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshtushwa na madai ya madereva wa Serikali kulogana ili wapate magari ya kufanyia kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Juma Mtanda kwenye kongamano la tatu la madereva wa Serikali la mwaka 2024 linaloendelea jijini Arusha kwa siku nne mfululizo.

Mtanda amesema baadhi ya madereva wamekuwa wakilogana ili wapate magari ya kuendesha kutokana na vyombo vyao kuharibika na kuishia kukaa kwenye ajira wakilipwa mishahara bila kupangiwa majukumu, hivyo baadhi hufanya mambo hayo wapangiwe kazi.

Akizungumzia leo Agosti 20, 2024, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wakuu wote wa taasisi na waajiri kuhakikisha wanafanya tathimini ya magari yote ya Serikali yaliyoharibika na yatengenezwe, kuhakikisha madereva wote walioajiriwa wanapata vyombo vya kufanyia kazi.

"Mmh! hili la kulogana limenishtua sana, sijawahi kujua kwamba madereva mnafikia hatua ya kulogana ili mpate vyombo vya kufanyia kazi.”

"Hivyo sasa nitumie nafasi hii, kuwaagiza wakuu wote wa taasisi na waajiri waanze kufanya tathimini mapema sana ya kufufua magari ya Serikali yaliyoharibika ili madereva wapangiwe kazi wasilogane kugombea machache yaliyopo," amesema.

Mbali na hilo, amewataka waajiri kubainisha madereva waliopo kwenye taasisi zao ambao hawana vyombo vya kufanyia kazi au hawajapangiwa majukumu, ili Serikali iwatambue na kuwapangia kazi.

Chanzo: Mwananchi
 
Imagine hiyo ni thinking ya mkuu wa mkoa!! Nenda hivyo hivyo na hii chain hadi kwa aliyemteua.....

Jaribu kuunganisha hii thinking na ubunifu...kujituma....kujitathmini na kuwajubuka..... imagine tena na tena ndo utajua kwanini Afrika baada ya mkoloni tumerudi nyuma zaidi badala ya kwenda mbele!!

Tuna kizazi cha hovyo sana!
 
Waziri mkuu anastushwa na nn hapo? Unadhani Mwigulu Nchemba kuendelea kubakia ofisini hadi leo, kabakia hivi hivi?
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshtushwa na madai ya madereva wa Serikali kulogana ili wapate magari ya kufanyia kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Juma Mtanda kwenye kongamano la tatu la madereva wa Serikali la mwaka 2024 linaloendelea jijini Arusha kwa siku nne mfululizo.

Mtanda amesema baadhi ya madereva wamekuwa wakilogana ili wapate magari ya kuendesha kutokana na vyombo vyao kuharibika na kuishia kukaa kwenye ajira wakilipwa mishahara bila kupangiwa majukumu, hivyo baadhi hufanya mambo hayo wapangiwe kazi.

Akizungumzia leo Agosti 20, 2024, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wakuu wote wa taasisi na waajiri kuhakikisha wanafanya tathimini ya magari yote ya Serikali yaliyoharibika na yatengenezwe, kuhakikisha madereva wote walioajiriwa wanapata vyombo vya kufanyia kazi.

"Mmh! hili la kulogana limenishtua sana, sijawahi kujua kwamba madereva mnafikia hatua ya kulogana ili mpate vyombo vya kufanyia kazi.”

"Hivyo sasa nitumie nafasi hii, kuwaagiza wakuu wote wa taasisi na waajiri waanze kufanya tathimini mapema sana ya kufufua magari ya Serikali yaliyoharibika ili madereva wapangiwe kazi wasilogane kugombea machache yaliyopo," amesema.

Mbali na hilo, amewataka waajiri kubainisha madereva waliopo kwenye taasisi zao ambao hawana vyombo vya kufanyia kazi au hawajapangiwa majukumu, ili Serikali iwatambue na kuwapangia kazi.

Chanzo: Mwananchi
Huyu mkuu wa mkoa ajiuzuru haraka imemuonyesha ni mtu wa aina gani au atenguliwe, amejuaje hayo mambo maana kama wanafanya siku zote ni siri zao nani atasema anaroga wenzake. Huyu jamaa ni mshirikina na serikali siku zote haikubali hizi imani anakuja anaogea hadharani ujinga huu, hawa ndio wanachochea kukata watoto ma albino.
 
Serikali si haiamini uchawi? Au nakosea watu wangu

Back
Top Bottom