Waziri mkuu kumwakilisha Rais Samia katika mkutano wa kimataifa wa Norman E. Borlaug Marekani

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameondoka nchini leo, Jumamosi, Oktoba 17, 2026, kuelekea jijini Des Moines, Jimbo la Iowa, nchini Marekani, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug (Borlaug Dialogue), utakaofanyika kuanzia Oktoba 20 hadi 22, 2026.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu anatarajiwa kutoa hotuba kuu na kushiriki majadiliano kuhusu maendeleo ya kilimo, usalama wa chakula na matumizi ya teknolojia katika kuongeza tija, huku akieleza vipaumbele vya Tanzania na kutangaza fursa za biashara na uwekezaji katika sekta ya kilimo.

Waziri Mkuu pia anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Taasisi ya Tuzo ya Chakula Duniani (World Food Prize Foundation) na Muungano wa Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA), pamoja na wadau wa biashara na uwekezaji katika kilimo.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali chini ya uongozi wa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kuimarisha diplomasia ya uchumi na kuvutia uwekezaji na teknolojia katika kilimo ili kuongeza uzalishaji, ajira na kipato cha wananchi katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
 
Kwa hiyo huku ndio anabaki makonda kujikweza
Roho inamuuma HAWEZ kwenda AMERIKA
 
π—ͺπ—”π—­π—œπ—₯π—œ π— π—žπ—¨π—¨ π—žπ—¨π— π—ͺπ—”π—žπ—œπ—Ÿπ—œπ—¦π—›π—” π—₯π—”π—œπ—¦ π——π—žπ—§. π—¦π—”π— π—œπ—” π—žπ—”π—§π—œπ—žπ—” π— π—žπ—¨π—§π—”π—‘π—’ π—ͺ𝗔 π—žπ—œπ— π—”π—§π—”π—œπ—™π—” π—ͺ𝗔 𝗑𝗒π—₯𝗠𝗔𝗑 π—˜. 𝗕𝗒π—₯π—Ÿπ—”π—¨π—š 𝗠𝗔π—₯π—˜π—žπ—”π—‘π—œ

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameondoka nchini leo, Jumamosi, Oktoba 17, 2026, kuelekea jijini Des Moines, Jimbo la Iowa, nchini Marekani, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug (Borlaug Dialogue), utakaofanyika kuanzia Oktoba 20 hadi 22, 2026.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu anatarajiwa kutoa hotuba kuu na kushiriki majadiliano kuhusu maendeleo ya kilimo, usalama wa chakula na matumizi ya teknolojia katika kuongeza tija, huku akieleza vipaumbele vya Tanzania na kutangaza fursa za biashara na uwekezaji katika sekta ya kilimo.

Waziri Mkuu pia anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Taasisi ya Tuzo ya Chakula Duniani (World Food Prize Foundation) na Muungano wa Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA), pamoja na wadau wa biashara na uwekezaji katika kilimo.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali chini ya uongozi wa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kuimarisha diplomasia ya uchumi na kuvutia uwekezaji na teknolojia katika kilimo ili kuongeza uzalishaji, ajira na kipato cha wananchi katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
 

Attachments

  • IMG-20261017-WA0147.jpg
    277.7 KB · Views: 7
  • IMG-20261017-WA0155.jpg
    391.3 KB · Views: 6
  • IMG-20261017-WA0153.jpg
    256.1 KB · Views: 5
  • IMG-20261017-WA0149.jpg
    357.8 KB · Views: 6
  • IMG-20261017-WA0151.jpg
    259.1 KB · Views: 5
Mbona Samia haendi tena Ulaya na Marekani kama zamani?
 
the only positive thing, nimeona yuko na mke wake na tabasamu kubwa, maana yake is a family man na anamthamini mke wake, a happy woman, a happy man, Mungu aibariki familia yao ...
 
Mkutano tarehe 20 yeye anaondoka Leo tarehe 17 kwani amesafiri kwa kutumia 'basi' au amewahi mahemezi kwanza ndo akasinzie kwenye mkutano ukiisha arudi bongolala?
 
Kila la kheri baba,
unafanya kazi kubwa na nzuri sana kwa niaba ya Rais na waTanzania wote baba PM Dr Mwigulu Nchemba πŸ’ͺ
 
Huyo maza aliyevaa miwani akikusikia unazungumuzia kuhusu no reforms no election kukuua ni nje nje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…