Waziri Mkuu Majaliwa ameamua kumsaidia Rais Samia kwa vitendo kuliko maneno

Waziri Mkuu Majaliwa ameamua kumsaidia Rais Samia kwa vitendo kuliko maneno

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Ni takribani Mwaka wa 2 sasa tangu Serikali ya Awamu ya 6 iingie Madarakani. Serikali iliyojipambanua kwa kufungua mipaka na kuichora upya ramani ya Tanzania kwenye ramani ya dunia. Katika safari hii yenye mafanikio makubwa na matumaini kwa Watanzania, Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan , Makamu wa Rais Dr.Mpango na Waziri Mkuu Majaliwa K. Majaliwa wamekuwa mifano ya kuigwa kwa hatua za kiutendaji wanazozichukua kila kukicha.

Pamoja na uwezo huo unaoneshwa na Viongozi hawa, hivi sasa nchini kumetokea tabia ya ajabu kabisa ambayo inafanywa na watu waliopata jina pendwa la MACHAWA🕷️🕷️🕷️🕷️ yaani wala Rushwa . Machawa hawa wameamua kujipa kazi moja tu ya kusambaza chuki baina ya Viongozi ili Viongozi wetu watofautiane na washindwe kufanya kazi kwa ushirikiano na kuaminiana. TUMEWASHTUKIA na hamtafanikiwa kwa kuwa agenda zenu zote tunazijua.

Hivi majuzi Mama akiwa kwenye Mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi alisikika akiahidi kuipanga Serikali yake upya kwa sababu aliyoitaja kuwa wapo watu kwenye Serikali yake wasioendana na kasi yake. "Sisi wananchi tunakubaliana na Mama kabisa kwamba kuna watu hawaendani na kasi yake na sisi wananchi tunamuunga mkono kuchukua hatua maana ndio hao wanaomrudisha nyuma yeye na Serikali.” Inashangaza sana unakuta kwenye Sekta mbalimbali kuna madudu na mawaziri husika wapo na Viongozi wa ngazi za Mkoa ,Wilaya na Wakurugenzi wa Almashauri wapo ila wanasubiri Waziri Mkuu afanye ziara ndio yagundulike madudu, hii si sawasawa na ndio maana tunaunga mkono nia ya mama ya kufanya mabadiliko.
Hata hivyo, MACHAWA wametafsiri wanavyotaka wao kwa nia zao ovu, wakiwa na mpango wao wa kuendeleza NONGWA mitandaoni.

Wapo MACHAWA wanaojenga hoja kuwa Waziri Mkuu hatakiwi kukaa muda mrefu kwenye Serikali . Kiufupi hoja yao hii haina msingi wowote, ebu tujikumbushe kidogo
mifano kutoka hapa nchini na nchi zilizoendelea hasa Uingereza, ambako Robert Walpole Waziri Mkuu wa Uingereza aliekaa muda mrefu zaidi alieongoza Serikali kwa miaka 21, lakini pia hapa nchini tunae Waziri mkuu mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye aiehudumu kwa miaka 10, kwakuwa kinachoangaliwa ni utendaji wake na namna anavyomsaidia kazi Rais wake.

Waziri Mkuu ambae ni mtendaji mkuu serikalini amekuwa akiendeleza kasi yake ile ile ya kiutendaji kila kukicha, na ambaye kupitia ziara zake amekuwa akiibua mambo mbalimbali kama vile utendaji usioridhisha kwa baadhi ya watumishi na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa baadhi ya maeneo mbalimbali nchini.

Tunafahamu ya kwamba kwa miaka 2 ya Mhe. Samia fedha nyingi zimepelekwa maeneo mbalimbali nchini kutekeleza miradi ya maendeleo na mara kwa mara amekuwa akisisitiza uadilifu katika matumizi ya fedha hizo. Na ndio maana Waziri Mkuu wake amekuwa mkali katika kufatilia matumizi ya fedha hizo.Waziri Mkuu ameibua na kuweka wazi ufujaji wa pesa za Serikali kwenye miradi ya maendeleo na katika maeneo baadhi ya utendaji, na hata kuikataa miradi ambayo hakuridhishwa na utendaji wake mzalendo huyu. Mara kadhaa kupitia mikutano yake Mhe. Dr. Samia Suluhu Hasan Rais wetu ,amekuwa akionya vikali utendaji mbovu, wizi wa fedha za umma, miradi isiyokidhi viwango na kwamba wale wote watakaojihusisha atawaonyesha rangi zake. Hivyo anachokifanya waziri Mkuu ni kutekeleza maagizo . Niukweli usiopingika kwamba hatua zinazochukuliwa ndizo wananchi tunazotaka kuziona zikichukuliwa na Viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kutuongoza.

Wakati MACHAWA wanamwaga sifa za kujipendekeza kwa maneno bila vitendo, ni kipindi hicho hicho mchapa kazi PM yupo bize na maswala ya msingi kwenye utendaji AKIMSAIDIA MAMA KWA VITENDO, ameibua madudu ya baadhi wa watumishi wanaofuja fedha na mali za umma kupitia ziara zake .

Sisi watanzania tunamwelewa Waziri Mkuu na dhamira yake njema ya utendaji na KUMSAIDIA Mheshimiwa Rais majukumu yake kuliko hao wanaoshinda mitandaoni wakiwachonganisha viongozi. Watanzania tunaona na tuna macho, tunanajua ni nani anawajibika katika majukumu yake kumsaidia Rais na ni nani yupo bize kusaka madaraka 2025. Waziri Mkuu ni mchapa kazi na kazi lazima ziendelee.

Wananchi tunapenda kuona watu wenye uchungu na rasilimali za taifa, watu wenye matendo kuliko maneno, watu wanaojua mahitaji ya nchi kwa sasa. Tunahitaji kuona RUSHWA inapungua/inaisha, tuwe na UMEME, MAJI, na VITUO vya AFYA, Taifa hili la uwekezaji linahitaji umeme wa uhakika na sio mgao usioisha.

MACHAWA TUSIKILIZANE “Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wake Dkt. Mpango, na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa ni mpango wa Mungu” na wana nia ya dhati ya kulikomboa taifa hili. Sisi wananchi tunasimama na Mama na Wasaidizi wake wote wenye nia njema na nchi yetu kwa umoja wao na KAZI IENDELEE…..

Mwananchi
Issa Mkuya
 

Attachments

  • Screenshot_20221219-124757.jpg
    Screenshot_20221219-124757.jpg
    16 KB · Views: 6
Kwani hao watendaji waliwekwa na Chadema? Hakuna msafi ndani ya Ccm
 
Ni Sarakasi za kisiasa tu , tujiulize wakuu wa mikoa RC, RAS, DC, DAS, DED n.k hawaoni mapungufu ktk maeneo yao ya kiuongozi ya utawala hadi mheshimiwa waziri mkuu anafika na kuyabaini kwa mara ya kwanza .

Je wateule wote wa rais ngazi za mikoa na wilaya inakuwa vipi hawaoni haya mapungufu ktk mikoa na wilaya je muda wote kazi yao ni ipi?

Tukisoma historia ya ma-DC wa mkoloni na majukumu yake tunaona kuwa walijitayarisha kwenda kufanya kazi mikoani / wilayani kwa kina kabisa lengo ni wao katika kipindi cha utumishi wao ndani ya eneo husika kutatua kero, changamoto na kuwa kichocheo cha wananchi kusimamia na kujiletea maendeleo katika ngazi ya wilaya na mikoa wanayoishi badala ya kutegemea utatuzi wote utoke Dodoma na Dar es Salaam .


SHAJARA ZA DC WA MKOLONI NCHINI TANGANYIKA.

1671445178789.png

For example, the President of the Republic of Tanzania said not long ago, “The colonial government had no intention of developing the country but just wanted to exploit its resources.” His views appear to be shared by some commentators in this country, and even by authoritative voices in places like the BBC and the Times newspaper.

These criticisms sadden me. Our colonial administration deserves to be given a fair hearing, and our work to be assessed even-handedly. For this reason, should these pages ever reach a wider readership beyond the family, I have put on the record some detail of my work and leisure to enable readers to judge for themselves. I have tried to avoid hindsight and those loose generalisations that hide reality, nor have I relied on my memory which is rose-tinted and wholly unreliable after sixty years

In my letter of appointment, I had been told the Course would cover the following broad subjects, on which I would be examined at the end of it: Colonial History, Colonial Government, Criminal Law and the Law of Evidence, Land Use in the Tropics, Social Anthropology, Economics and most importantly, the Swahili language.

Tanganyika

I also read as much as I could find about the system of administration in Tanganyika. It had been developed by Lord Lugard in West Africa and Sir Donald Cameron in the East, and was known as ‘Indirect Rule’. Chiefs, and federations of chiefs, were recognised to run local government through their tribal structures of petty chiefs and headmen. Their Native Authorities raised their own revenue from fees and taxes to spend on local development and administration, while native courts were empowered to settle civil and minor disputes. The DC had ultimate authority while supporting and advising the system. He was also a magistrate with significant powers in criminal cases; he had responsibility in most areas for the police and prisons; and he was Head of the District Team which could include specialist European staff with duties concerning agriculture, animal health, construction, nursing and medicine. In each district the DC could normally dispose of one or two District Officers (DOs), of whom the junior was often a newly-fledged Cadet which I was to become.

It was necessary to learn about the country in which I was to serve. The Germans had occupied Tanganyika in the 1880s during the so called ‘Scramble for Africa’, had brought law and order to the country, building forts known as ‘Bomas’ in all the population centres, ending the mainland slave trade, and putting down rebellions with great severity...
....

READ MORE :
Source : The Memoirs of Dick Eberlie, District Officer in the Colonial Service in Tanganyika (renamed Tanzania in 1964).
 
Back
Top Bottom