Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameagiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha madarasa ya mpango wa elimu ya msingi kwa waliokosa (Memkwa) yanafufuliwa.
Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatano Juni 9, 2021 wakati akizindua Kongamano la kimataifa la miaka 50 ya elimu ya watu wazima lenye kauli mbiu ya ‘elimu ya watu wazima kwa maendeleo endelevu’.
Amesema kwa kufanya hivyo itapunguza ongezeko la watu wazima wasiojua kusoma na kuandika pamoja na kuwasaidia waliokosa nafasi ya kupata elimu waweze kuipata.
“Pia tumieni madarasa hayo kuwezesha watu wazima wapate stadi mbalimbali pamoja na stadi za KKK. Lakini pia naagiza halmashauri zote zitenge fedha kwaajili ya walimu wanaojitolea kufundisha madarasa hayo, pamoja na taasisi yenyewe iandae walimu na kuwa na idadi yao.”
“Sasa hivi tunaona kuna vijana wengi wamemaliza vyuo vikuu vya ualimu kwa ngazi ya diploma na vyeti hawajaingia kwenye ajira hivyo hawa wanaweza kutumika,” amesema.
Pia, amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha programu hizo zinakuwepo na kusimamia uwepo wa madarasa kwa watu watakaojitokeza pamoja na idadi yao.