Waziri Mkuu Majaliwa: Disemba 31, 2024 siku ya mwisho kwa matumizi ya Mkaa na Kuni Taasisi za Umma

Waziri Mkuu Majaliwa: Disemba 31, 2024 siku ya mwisho kwa matumizi ya Mkaa na Kuni Taasisi za Umma

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amezikumbusha Taasisi na mashirika yote ya Serikali yaliyopo kote nchini Tanzania ambayo yanahudumia watu zaidi ya 100, kutekeleza bila shuruti agizo lake la kuitangaza Disemba 31, 2024 kuwa siku ya mwisho kwa matumizi ya Mkaa na Kuni kwenye shughuli za Mapishi.

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa ametoa kauli hiyo mapema Leo Jumanne Disemba 31, 2024 wakati akihutubia wananchi kwenye Tamasha la Azimio la Kizimkazi 2024, linalofanyika kwa mara ya pili Ruangwa Mkoani Lindi ikiwa ni mara baada ya kuzinduliwa kwake mapema mwaka huu na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kizimkazi Visiwani Zanzibar.

Soma Pia: Waziri Mkuu aipongeza DAWASA kuchagiza matumizi ya nishati safi

Waziri Mkuu amezitaja taasisi zinazohusika na agizo hilo kuwa ni pamoja na Taasisi zote zenye kuhudumia watu zaidi ya mia moja ikiwemo Majeshi mbalimbali, Shule za bweni za Binafsi na za serikali, Magereza pamoja na Wazabuni wanaopika vyakula vya zaidi ya watu 100 ambapo lengo ni kufikia mwaka 2034, asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia ili kuondokana na athari za kiafya na uharibifu wa misitu unaotokana na matumizi ya kuni na Mkaa.

Katika kutekeleza Lengo hilo la mwaka 2034, Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri zote nchini Tanzania kuhakikisha kuwa ajenda ya matumizi ya nishati safi inakuwepo kwenye mikutano na shughuli zao mbalimbali kwa kutoa hamasa kwa wananchi juu ya faida ya matumizi ya nishati safi na athari za matumizi ya nishati chafu ya kupikia.

Waziri Mkuu ametaja uwepo wa magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya macho, Pumu, mapafu, maumivu ya kifua na magonjwa ya moyo kama miongoni mwa athari zinazowakumba kinamama na wasichana wengi kutokana na kutumia kuni na mkaa kwenye kupika vyakula.
 
Itakuwa hatua nzuri. Changamoto ni utekelezaji maana hii nchi kwa matamko tu tupo vizuri.
 
Hii nchi ni vituko, hizo taasisi mfano shule zinafunguliwa majiko yaliyopo ni ya kuni halafu mwisho leo kutumia hayo majiko!

Halafu huyu waziri si alisema Raisi ni mzima wa afya yupo anachapa kazi halafu anaongea hayo akiwa msikitini.
Ukweli mimi huwa naona hakuna la maana analoongea huyu waziri.
 
Hio gesi inayopigiwa chapuo ambayo inasafiriwa kwa meli kutoka ughaibuni ndio haichafui mazingira ? Au hayo mashule ambayo yataanza kutumia hio LPG hivyo gharama kuongezeka na Karo wazazi kulipia kuongezeka ? Au tutatumia Kodi zetu kutoa Ruzuku ili bei ipungue na tuagize LPG hio kutoka ughaibuni ?

 
Back
Top Bottom