Waziri Mkuu Majaliwa: Hatutomwacha DP World aende zake

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Katika mkutano na wananchi wa mjini Mtwara juzi, Majaliwa alisisitiza kuwa hadi sasa kilichotiwa saini ni makubaliano ya awali na muda ukifika maoni ya wananchi yatazingatiwa.

“Hatuwezi kumwacha huyu (DP World) aende zake. Kilichopitishwa na Bunge si mkataba wa miradi ni makubaliano ya awali baina ya nchi ili kuruhusu uwapo wa mikataba ya miradi husika, hivyo katika mikataba hiyo maoni yenu yatazingatiwa,” alisisitiza.

Akifafanua baadhi ya hoja zinazotolewa na wanaopinga makubaliano hayo, Majaliwa alisema “maeneo ambayo mna shaka nayo, mnasema mkataba huu ni wa kudumu, sisi tunasema bado. Kwenye mkataba huo tutaweka muda wa kumfanyia tathmini (mwekezaji) aendelee au la, kwa sababu hata huyo aliyeondoka mwaka jana naye tulimpa muda wa vipindi mpaka akafikia miaka 22.

“Uwekezaji pale (bandarini) siyo suala geni, siyo kitu kipya. Mmesema tuzingatie maslahi ya Taifa, ninataka niwahakikishie kwamba mkataba utazingatia maslahi ya taifa hili. Serikali yenu ni sikivu,” alisema.

Akijibu hoja ya ardhi kwamba mwekezaji huyo ameichukua, kiongozi huyo alisema "mmesema ardhi ameichukua, itakuwa ya kwake… hapana! Hakuna mwekezaji aliyepewa ardhi, hata sheria za uwekezaji, mwekezaji hapewi ardhi, bali anapata kibali cha kukaa juu ya ardhi na akikaa hapo atalipa kodi,” alifafanua.

Kuhusu muda wa mkataba ambao baadhi ya wadau walisema mwekezaji huyo amepewa kwa miaka 100 na wengine miaka yote, Majaliwa alikanusha na kusema halijatamkwa kokote.

Alisisitiza mwekezaji huyo atakapokuja watakubaliana miaka ya kukaa na kufanya tathimini kama ni miaka mitano kisha mitano tumwangalie au kama ni miaka 10.

Akifafanua hoja ya watu kupoteza ajira, Majaliwa alisema hakuna mtumishi wa bandari ambaye atapoteza ajira yake.

“Hofu nyingine wamesema serikali haitapata hata senti tano kwa hiyo huyo anakuja kukaa hapa anaondoka hatupati hata senti tano. Kwani sisi hatuwezi kusimamia maslahi ya watanzania kweli? Huyu tumlete hapa asilipe hata senti tano kweli? Haiwezekani lazima alipe kodi.

“Watanzania wenzangu tuamini jambo hili linakokwenda litaleta maslahi kwa taifa na serikali itazingatia maslahi ya watanzania. Tatizo ni kwamba watu wanasema bandari yote, siyo kweli.

“Sisi tunalenga sehemu ya kupakia na kushushia. Meli nyingi zinashindwa kuingia pale kwa sababu mitambo tuliyonayo ni midogo midogo ya kushusha na kupakia, haishushi kwa haraka,” alifafanua.

Majaliwa alisisitiza kuwa hakuna mahala wanataka kudhuru watanzania na kuomba waiamini serikali kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ana nia njema ya kufungua milango kiuchumi.

“Maeneo haya matano yenye wasiwasi tunayafanyia kazi kwa hiyo kilichopitishwa na wabunge si mkataba na DP World, bali makubaliano ya nchi na nchi ili kuruhusu kuzungumza,” alifafanua.

Alisema serikali inatarajia kujenga reli ya kisasa (SGR) ambayo itaunganisha Bandari ya Mtwara na mikoa mingine ili kuufungua ushoroba wa mkoa huo.

“Tutajenga reli ili kuiunganisha bandari yetu na migodi ya makaa ya mawe kule Liganga, Nchuchuma na nyingine itakwenda Iringa ili kuifungua Mtwara," alisema.

Mbunge wa Mtwara Mjini, Hassan Mtenga, aliiomba serikali kuhakikisha korosho zinasafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

“Kuna vijana tangu saa 12 asubuhi hadi saa sita usiku wako kwenye makundi ya mtandaoni (WhatsApp) kutukana viongozi, hili ni kwa sababu hawana kazi ya kufanya.

"Iwapo korosho zetu zitasafirishwa kupitia bandari yetu, vijana hawa watapata ajira na kuacha kutukana viongozi,” alisema.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, alisema serikali imewekeza zaidi ya Sh. bilioni 157 kutekeleza mradi ujenzi wa gati jipya la Bandari ya Mtwara.

“Uwekezaji huu umelenga kuifanya Bandari ya Mtwara kuwa ya kimkakati na sasa inaweza kufunga meli zaidi ya nne kwa wakati mmoja. Haya ni maendeleo makubwa,” alisema.

Waziri wa Ofisi ya Rais - Kazi Maalum, Kapteni mstaafu George Mkuchika, aliwataka wananchi wa Mtwara kutoyaogopa mabadiliko ya uendeshaji wa bandari na badala yake waiunge mkono serikali.

“Msiogope na wala msiwe na wasiwasi, ni tabia ya mwanadamu kuogopa mambo mapya, suala la uwekezaji katika bandari siyo geni,” alisema Mkuchika.

Majaliwa yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi na jana alitembelea Halmashauri ya Mtwara na Mji wa Nanyamba.

Chanzo: Nipashe
 
Kwani Majaliwa leo yuko Mtwara? Mbona kama yuko Dodoma?
 
Wanaopinga uwekezaji bandarini ni wajinga, nchi itafaidika sana kiuchumi
Wee chawa uliekunywa maji ya bendera usipotoshe!! Hakuna mtanzania anaepinga uwekezaji nchini, refer kauli ya PM mapendekezo ya watanzania yataganyiwa kaz means kuna some articles kweny mkataba ndizo zenye ukakasi na sio huu upotoshaji wako!!
 
Wanashangaza sana wanapoamua kutumia miguvu kama madikteta, kama mmeshindwa kujibu maswali ya watanganyika kuhusu huo uwekezaji wa mwarabu wa kinyonyaji msijidanganye kwa kulazimisha, hii nchi sio ya viongozi, ni ya watanganyika, tuheshimiane.
 
Kwani kujibu Hoja kwa Hoja kuna shida gani kwa ma dalali?
 
Mungu anasema na Mh majaliwa na waziri mkuu kwamba , kamwe hii kampuni kabidhiwa bandari kwa njia hizi,haitawezekanika period, na namuomba popote alipo azingatie neno hili , na kumshauri boss wake mapema, naishia hapa,

Sasa yangu macho kwamba Mungu aniache niabike mbele ya mwanadam mh Majaliwa ,kwangu itakua ya kwanza maana naamini Mungu wangu yupo up to date sana , stop hii kitu
 
Sasa watanganyika wajiandae kukabiliana na bandari .
Tutayaanzisha yale ya Raila mwrzi mzima mikoa yote , wilaya zote
 
Hivi account za hawa watu zinasoma ngapi?
Kwa nguvu inayotumika, si bure!!

Imagine Msukuma kavuta VX, Kitenge Kavuta Shangingi, Steve Nyerere anasafirishwa Business class .... Sasa hapo Maza, Tulia na Majaliwa itakuwaje!!? Hapo ni common sense tu....!!
 
Katika mkutano na wananchi wa mjini Mtwara juzi, Majaliwa alisisitiza kuwa hadi sasa kilichotiwa saini ni makubaliano ya awali na muda ukifika maoni ya wananchi yatazingatiwa.

“Hatuwezi kumwacha huyu (DP World) aende zake. Kilichopitishwa na Bunge si mkataba wa miradi ni makubaliano ya awali baina ya nchi ili kuruhusu uwapo wa mikataba ya miradi husika, hivyo katika mikataba hiyo maoni yenu yatazingatiwa,” alisisitiza.

Akifafanua baadhi ya hoja zinazotolewa na wanaopinga makubaliano hayo, Majaliwa alisema “maeneo ambayo mna shaka nayo, mnasema mkataba huu ni wa kudumu, sisi tunasema bado. Kwenye mkataba huo tutaweka muda wa kumfanyia tathmini (mwekezaji) aendelee au la, kwa sababu hata huyo aliyeondoka mwaka jana naye tulimpa muda wa vipindi mpaka akafikia miaka 22.

“Uwekezaji pale (bandarini) siyo suala geni, siyo kitu kipya. Mmesema tuzingatie maslahi ya Taifa, ninataka niwahakikishie kwamba mkataba utazingatia maslahi ya taifa hili. Serikali yenu ni sikivu,” alisema.

Akijibu hoja ya ardhi kwamba mwekezaji huyo ameichukua, kiongozi huyo alisema "mmesema ardhi ameichukua, itakuwa ya kwake… hapana! Hakuna mwekezaji aliyepewa ardhi, hata sheria za uwekezaji, mwekezaji hapewi ardhi, bali anapata kibali cha kukaa juu ya ardhi na akikaa hapo atalipa kodi,” alifafanua.

Kuhusu muda wa mkataba ambao baadhi ya wadau walisema mwekezaji huyo amepewa kwa miaka 100 na wengine miaka yote, Majaliwa alikanusha na kusema halijatamkwa kokote.

Alisisitiza mwekezaji huyo atakapokuja watakubaliana miaka ya kukaa na kufanya tathimini kama ni miaka mitano kisha mitano tumwangalie au kama ni miaka 10.

Akifafanua hoja ya watu kupoteza ajira, Majaliwa alisema hakuna mtumishi wa bandari ambaye atapoteza ajira yake.

“Hofu nyingine wamesema serikali haitapata hata senti tano kwa hiyo huyo anakuja kukaa hapa anaondoka hatupati hata senti tano. Kwani sisi hatuwezi kusimamia maslahi ya watanzania kweli? Huyu tumlete hapa asilipe hata senti tano kweli? Haiwezekani lazima alipe kodi.

“Watanzania wenzangu tuamini jambo hili linakokwenda litaleta maslahi kwa taifa na serikali itazingatia maslahi ya watanzania. Tatizo ni kwamba watu wanasema bandari yote, siyo kweli.

“Sisi tunalenga sehemu ya kupakia na kushushia. Meli nyingi zinashindwa kuingia pale kwa sababu mitambo tuliyonayo ni midogo midogo ya kushusha na kupakia, haishushi kwa haraka,” alifafanua.

Majaliwa alisisitiza kuwa hakuna mahala wanataka kudhuru watanzania na kuomba waiamini serikali kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ana nia njema ya kufungua milango kiuchumi.

“Maeneo haya matano yenye wasiwasi tunayafanyia kazi kwa hiyo kilichopitishwa na wabunge si mkataba na DP World, bali makubaliano ya nchi na nchi ili kuruhusu kuzungumza,” alifafanua.

Alisema serikali inatarajia kujenga reli ya kisasa (SGR) ambayo itaunganisha Bandari ya Mtwara na mikoa mingine ili kuufungua ushoroba wa mkoa huo.

“Tutajenga reli ili kuiunganisha bandari yetu na migodi ya makaa ya mawe kule Liganga, Nchuchuma na nyingine itakwenda Iringa ili kuifungua Mtwara," alisema.

Mbunge wa Mtwara Mjini, Hassan Mtenga, aliiomba serikali kuhakikisha korosho zinasafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

“Kuna vijana tangu saa 12 asubuhi hadi saa sita usiku wako kwenye makundi ya mtandaoni (WhatsApp) kutukana viongozi, hili ni kwa sababu hawana kazi ya kufanya.

"Iwapo korosho zetu zitasafirishwa kupitia bandari yetu, vijana hawa watapata ajira na kuacha kutukana viongozi,” alisema.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, alisema serikali imewekeza zaidi ya Sh. bilioni 157 kutekeleza mradi ujenzi wa gati jipya la Bandari ya Mtwara.

“Uwekezaji huu umelenga kuifanya Bandari ya Mtwara kuwa ya kimkakati na sasa inaweza kufunga meli zaidi ya nne kwa wakati mmoja. Haya ni maendeleo makubwa,” alisema.

Waziri wa Ofisi ya Rais - Kazi Maalum, Kapteni mstaafu George Mkuchika, aliwataka wananchi wa Mtwara kutoyaogopa mabadiliko ya uendeshaji wa bandari na badala yake waiunge mkono serikali.

“Msiogope na wala msiwe na wasiwasi, ni tabia ya mwanadamu kuogopa mambo mapya, suala la uwekezaji katika bandari siyo geni,” alisema Mkuchika.

Majaliwa yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi na jana alitembelea Halmashauri ya Mtwara na Mji wa Nanyamba.

Chanzo: Nipashe
Unaachaje pesa harafu uambulie empty words za kina kina Lisu na wapuuzi wengine 😂😂
 
Back
Top Bottom