Waziri Mkuu Majaliwa: Mhandisi, Afisa Elimu Sekondari, Mkurugenzi nawasimamisha kazi, mnapelekwa Mahakamani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambana Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kushindwa kusimamia matumizi ya Fedha ujenzi wa Bwalo shule ya Sekondari ya Wasichana Lugalo.

Ashangazwa kutumika kwa fedha yote ya ujenzi wa Bwalo lakini mpaka sasa halijakamilika.

Your browser is not able to display this video.
Bwalo hilo lilipangiwa sh. milioni 774 na wamekwishatumia sh. milioni 341 hadi kufikia hatua ya linta ambayo ni sawa na asilimia 40 ya ujenzi wake.

Aagiza asimamishwe kazi kupisha uchunguzi, yumo pia Mkurugenzi Mstaafu wa Halmashauri aliyestaafu mwezi Aprili mwaka huu, ambapo Mheshimiwa Majaliwa aagiza aitwe na ahojiwe.

Mheshimiwa Majaliwa yupo mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi.
 
Siasa izo...Majibu kamili ni uchunguzi ukishakamilika alafu Pia Takukuru izo ndio kazi zao na ndio wakitoa Tamko ndio la kweli ila sio haya ya jukwaani
 
Upuuzi mtpu, mbona wa kwenye CAG reort wanatanua mtaani. Kuwaonea wasiokuwa na wa kuwatetea
 
Hata wa report ya CAG mngewapeleka ingekuwa poa sana.
 
System ndo mbovu, hayo matukio ni nchi nzima, boresheni mfumo wa kutoa pesa za maendeleo, tenda zisipewe ma kanda wa chama cha ccm.
 
Safi Sana majaliwa, Tamisemi uozo na upigaji mwingi Sana, inaumiza Kodi zetu zinatafunwa kipuuzi bila huruma
 
Hii nchi bhana,
Nusu ya pesa ishatafunwa na boma Hata halijaisha,Finishing sjui Hali itakuaje🤔
 
Amewashtukizia tu, ila ukiingia kwenye vitabu utakuta kila kitu kipo sawa.

Wa Tanzania wana ujuzi kwenye kuiba
 
Siasa izo...Majibu kamili ni uchunguzi ukishakamilika alafu Pia Takukuru izo ndio kazi zao na ndio wakitoa Tamko ndio la kweli ila sio haya ya jukwaani
uko sahihi ! Lakini taarifa za hivyo zinamuathiri mhusika moja kwa moja hata kwa mfano kama Mh Mkurugenzi alikua anaplan za kugombea Ubunge au nafasi nyingine yeyote hapo amekua amechafuka sana. Hata kama Takukuru wata mclear bado anabaki na doa kubwa sana ukizingatia hizo ni pesa za umma
 
Safi Sana majaliwa, Tamisemi uozo na upigaji mwingi Sana, inaumiza Kodi zetu zinatafunwa kipuuzi bila huruma
Wale waliotajwa na CAG walioiba mabilioni ya pesa amewafanya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…