Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema michango ya wadau waliojitolea kwenye tukio la maporomoko ya tope ilikidhi mahitaji ya kujenga nyumba zote za wahitaji 109 za waathirika wa maporomoko hayo ambayo yalipelekea vifo vya watu 89.
Nyumba hizo ambazo zimejengwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) zipo katika kijiji cha Wareti, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.