Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa, ameongeza miezi mitano ya ukomo wa matumizi ya nishati chafu iliyokuwa ikamilike Desemba mwaka jana, kwa Taasisi zinazohudumia watu zaidi ya mia moja kutumia nishati safi ili kuepukana na changamoto ya ukataji wa miti hovyo.