Waziri Mkuu Majaliwa: Wanunuzi wa tumbaku ambao hawajawalipa wakulima wachukuliwe hatua

Waziri Mkuu Majaliwa: Wanunuzi wa tumbaku ambao hawajawalipa wakulima wachukuliwe hatua

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
WANUNUZI WA TUMBAKU AMBAO HAWAJAWALIPA WAKULIMA WACHUKULIWE HATUA - MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza wanunuzi wote ambao wamechukua tumbaku za wakulima na hawajawalipa fedha zao wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani kwani Serikali inataka kuona wakulima wakinufaika na zao hilo.

“Tumbaku katika mkoa wa Tabora ni uchumi, hivyo viongozi kuanzia ngazi ya wizara, mkoa, wilaya, kata na hata vijiji simamieni ushirika kwenye maeneo yenu, ushirika ni uchumi. Sote tuwajibike kwa pamoja, tuhakikishe ushirika unapata mafanikio.”

Ametoa agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Septemba 9, 2022) wakati akizungumza na viongozi wa Vyama Vikuu vya Ushirika, AMCOS na wakulima wa tumbaku kutoka wilaya za Urambo na Kaliua, mkoani Tabora.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan haitasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayebainika kuhujumu ushirika nchini kwa sababu imedhamiria kuuboresha.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza wanunuzi wote ambao wamechukua tumbaku za wakulima na hawajawalipa fedha zao wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani kwani Serikali inataka kuona wakulima wakinufaika na zao hilo.
Ohooo! Yale Yale ya Magufuli kwenye korosho! Majaliwa anawatisha wanunuzi wa tumbaku. Wakisusa atatuma JWTZ wakaikusanye ili serikali inunue kama ilivyofanya kwenye zao la korosho 2018?

Nilitegemea afuatilie changamoto zilizowasibu wanunuzi hao na awahimize wawalipe wakulima badala ya kuanza kutoa maneno na amri za viisho.

Waziri mkuu wa kanchi masikini kanakotegemea tozo kama Tanzania anatoa vitisho vitisho vya nini?
 
Back
Top Bottom