Waziri Mkuu Pinda ageuka mbogo Dodoma-Na dharau juu

Mkuu mwanatanu, huyo ndiye Mizengo Pinda doing what he does best!
 
Kuwa na eneo kubwa hakumaanishi kila kitu kinachotaka kufanywa au kujengwa inabidi likatwe pori, mambo mengine kwa dili na hapo serikali imetenngeneza dili na ikajipima na kuona uwezo wa kuwalipa wananchi wa eneo hilo upo ,makubaliano yemekwenda na wananchi wamekubali na kama kulihitajika upannuzi wa chuo hivyo imeonekana ni urahisi kuipanua sehemu hiyo na kujaliza majengo na wananchi wakishalipwa wao watajua la kufanya na muhimu kuwa wao ndio watakaotumia eneo jipya kuanzisha makazi ,labda ni serikali baada ya kuwalipa ingehitajika pia kuwatengea eneo na kuwagaia bure na zaidi kuwahakikishia wanapewa kwa ramani za kisasa na kila mtu anahakikishiwa kupata eneo kubwa la kujenga ukiwemo uzio wa nyumba yake kiasi ataweza pia kupata nafasi ya kulima mboga mboga na nyanya na kuweka mifugo ya kuku na hata ng'ombe wawili wa maziwa wa kisasa.Natumai ni mawazo mazuri tu kwa serikali inapoamua kununua eneo linalokaliwa na wananchi kwa kujenga labda shule au hospitali.
 
Mkuu KKN ni vigumu kupata sehemu kubwa ya kuweza kufanya mradi unaohitaji eneo kubwa (kama huu wa chuo kikuu ama barabara mpya), kinachofanyika ni kupunguza usumbufu kwa wananchi kadiri iwezekanavyo....fanya ufanyalo lazima kuna watu wachache au vitu fulani vitaumia....unavoidable. Lazima tukubali kuna watu kiasi fulani wataumia ili kupisha miradi ya maendeleo. Wanalipwa fidia (japo kweli si kila kitu kinaweza kufananishwa na fedha) ili wahame.

Kukiwa na miradi ya maendeleo kuna watu wanapenyeza siasa ama masilahi yao binafsi. Inawezekana wananchi wale wamedanganywa kwamba kuna fungu kubwa sana limetolewa kwa ajili yao, then wakaamua kutikisa kiberiti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…